Akizungumza wakati wa hafla ya kutaja majina ya wateule hao, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Taifa la Habari (MCT), Pili Mtambalike alisema mchujo huo umefanywa na jopo la majaji lililoongozwa na mkufunzi na mhariri wa habari wa siku nyingi nchini, Gervas Moshiro.PICHA|MAKTABA
Dar es Salaam. Waandishi wa Habari wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) inayochapisha magazeti ya Mwananchi, Mwanaspoti na The Citizen wanaongoza katika orodha ya wateule wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari 2013 (Ejat 2013) kwa kuingiza majina 15 kati ya 76 ya wateule watakaotunukiwa zawadi zao Machi 14 mwaka huu.
Akizungumza wakati wa hafla ya kutaja majina ya wateule hao, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Taifa la Habari (MCT), Pili Mtambalike alisema mchujo huo umefanywa na jopo la majaji lililoongozwa na mkufunzi na mhariri wa habari wa siku nyingi nchini, Gervas Moshiro.
Mtambalike alisema washindi
watatunukiwa tuzo zao na Rais wa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki, Jaji Harold Nsekela katika hafla itakayofanyika Machi 14
mwaka huu jijini Dar es Salaam. Jumla ya kazi 907 ziliwasilishwa kwa
ajili ya kuwania tuzo hizo.
Alisema majaji walizipitia na
kupitisha kazi 101 ambazo ni pamoja na za magazeti (46), redio (39) na
televisheni (16) na kulingana na takwimu hizo, idadi ya kazi za redio
imeongezeka kutoka 21 za mwaka 2012 na magazeti kazi tano zaidi
zimeongezeka
Kazi za televisheni zimepungua kwa
idadi ya tatu kutoka 19 za mwaka 2012. Idadi ya kazi zilizopitishwa
katika mchujo wa majaji hao zimeongezeka kutoka 76 hadi 81, kiwango
ambacho ni sawa na ongezeko la asilimia 24.6.
Mtambalike alisema pia idadi ya
washiriki wanawake nayo imeongezeka kutoka washiriki 12 hadi 18 kwa
mwaka 2013, ongezeko ambalo ni sawa na asilimia 63.6. Alisema ili majaji
kuwapata wateule hao walilazimika kufanya kazi ya ziada kutokana na
ushindani uliokuwepo.
Kwa upande mwingine, kaimu mkurugenzi
huyo alisema, jopo la wataalamu chini ya uenyekiti wa mhariri wa siku
nyingi na mtalaamu wa masuala ya habari, Theophil Makunga, bado lipo
katika mchakato wa uteuzi wa jina linalostahili kushinda Tuzo ya Maisha
ya Mafanikio na Uandishi wa Habari (LAJA).
Waandishi wa Magazeti ya Mwananchi na
The Citizen ambao majina yao yametajwa katika wateule wa tuzo hizo kwa
mwaka 2013 ni pamoja na Fred Azzah, Florence Majani, Polycarp Machira,
Kalunde Jamal, Herieth Makweta, Beldina Nyakeke, Sheilah Sezzy, Elias
Msuya, Jacqueline Masinde na Athuman Mtulya.
Wengine ni Fidelis Felix, Kelvin
Matandiko, Phinias Bashaya, Zephania Ubwani, Mussa Juma.Waandishi hao wa
MCL wameongezeka kwa idadi ya mwandishi mmoja ikilinganishwa na idadi
ya wateule 14 wa tuzo zilizopita.
Chanzo,mwananchi.co.tz.
0 comments:
Post a Comment