Na Mwandishi Wetu, Mwananchi
Dar es Salaam. Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ikishirikiana na wadau wake kuanzia kesho wanatarajia kuanza kutoa huduma kwa saa 24, siku saba za wiki, mwaka mzima bila kupumzika.
Ofisa Uhusiano wa TPA, Janeth Zurangi alisema uamuzi huo ambao unakusudia kuongeza ufanisi wa bandari hiyo, umefikiwa baada ya wadau mbalimbali kutia saini mikataba ya utekelezaji kazi hiyi
Zurangi alisema ingawa kulikuwapo
mabishano kuhusu vipengele kadhaa ndani ya mkataba huo, wadau wote
walikubali kuanza kutoa huduma kila siku kwa saa 24 kuanzia Machi Mosi.
"Mwezi ujao utaratibu huo utaanza na
tunatarajia utakuwa na mafanikio makubwa. Hivi sasa mteja anaweza
kuchelewa kuchukua mzigo kwa sababu baadhi ya wadau hawajasaini vibali
husika," alisema.
Oktoba 14 mwaka jana, Waziri wa
Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe aliwataka wadau wengine wanaofanya kazi
na TPA kuanzisha utaratibu wa kufanya kazi kila siku, kwa kile
alichoeleza kutofanya hivyo kunakwamisha kasi ya uondoaji mizigo
bandarini.
Dk Mwakyembe alinukuliwa akisema:
"Bandari wanafanya kazi saa 24 kwa siku saba za wiki bila kupumzika,
lakini wenzetu wa TRA wao sikukuu na siku za mwisho wa juma wanalala
hali hii inaturudisha nyuma kimapato." Baadhi ya wadao waliosaini
mkataba huo ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Chama cha Wakala wa
Forodha na Uondoshaji Shehena Tanzania (Taffa)
0 comments:
Post a Comment