Profesa Alexander Songorwa
WAZIRI wa
Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu amemuondoa katika nafasi yake
Mkurugenzi wa Wanyamapori, Profesa Alexander Songorwa na kumteua Paul
Sarakikya kukaimu nafasi hiyo.
Kwa
mujibu wa taarifa yake aliyoitoa jana kwa vyombo vya habari, Nyalandu
alisema amechukua hatua hiyo kutokana na kutoridhishwa na utendaji wa
kazi wa idara hiyo katika mapambano dhidi ya ujangili, yanayoendelea
nchini.
“Aidha
hatua hii ni utekelezaji wa Azimio la Bunge lililotolewa Desemba 22,
mwaka jana lililotaka Mkurugenzi wa Wanyamapori kuwajibishwa kutokana na
tuhuma za uzembe na ukiukwaji wa haki za binadamu katika Operesheni
Tokomeza,” alisema.
Alisema
pia amemuondoa Mkurugenzi Msaidizi wa Matumizi Endelevu ya Wanyamapori,
Jafari Kidegesho na kumteua Dk Charles Mulokozi kuchukua nafasi hiyo.
Katika
mabadiliko hayo, Nyalandu pia alimteua Julius Kibebe kuwa Mkurugenzi
Msaidizi Uzuiaji- Ujangili huku Mkurugenzi Msaidizi Uzuiaji-Ujangili na
Takwimu, Nebbo Mwina akiendelea kushika nafasi hiyo.
Alisema Mkurugenzi Msaidizi wa Uendelezaji wa Wanyamapori, Herman Keiraryo naye anaendelea kushikilia wadhifa huo.
CHANZO:HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment