>>WANAHABARI WAITAKA MILAN KUBADILI JEZI ZAO ZILIZOANDIKWA: “IL CLUB PIU TITOLATO AL MONDO”!!!
CAF imetangaza kuwa Vigogo wa Egypt, Al Ahly, ambao Wikiendi hii wataivaa Yanga
kwenye Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Kwanza ya CAF CHAMPIONZ LIGI,
wamewapiku Vigogo wa Italy, AC Milan, kwa kuwa na Mataji mengi ya
Kimataifa Duniani.
Baada CAF kutoboa mafanikio ya Al Ahly,
huko Italy Wanahabari wameitaka AC Milan kuondoa Lebo ya Jezi zao
inayosomeka: “Il Club Piu Titolato Al Mondo” ikimaanisha “Klabu yenye
Mafanikio Makubwa Duniani” kwa vile Al Ahly sasa wana Mataji ya
Kimataifa 19 ukilinganisha na 18 ya AC Milan.
Wiki iliyopita, Al Ahly walinyakua Taji lao la 19 baada ya kuichapa Klabu ya Tunisia CS Sfaxien Bao 3-2 na kubeba CAF SUPER CUP.
Makamu Rais wa AC Milan, Adriano
Galliani, amesema wataomba msaada wa FIFA ili kuthibitisha Mataji ya Al
Ahly kabla hawajabadili Jezi zao kama Wanahabari walivyoshauri.
Nae Rais wa CAF, Issa Hayatou,
amewapongeza Al Ahly: “Hongera kwa Al Ahly kwa mafanikio haya ya
Kihistoria! CAF inasikia fahari kwa kuiweka Afrika kwenye Ramani ya
Dunia kwa mara nyingine. Hili ni jambo bora kwa Soka la Afrika na
linathibitisha hatua kubwa zilizofikiwa na hii itahamasisha Klabu
nyingine kufanya zaidi.”
MATAJI
AL AHLY-19:
-CAF Champions League 8 [1982, 1987, 2001, 2005, 2006, 2008, 2012, 2013]
-CAF Cup Winners’ Cup 4 [1984, 1985, 1986, 1993]
-CAF Super Cup 6 [2002, 2006, 2007, 2009, 2013, 2014]
-Afro-Asian Cup 1 [1988]
AC MILAN-18:
-UEFA Champions League 7
-UEFA Super Cup 5
-UEFA Cup Winners’ Cup 2
-Intercontinental Cup 3
-FIFA Club World 1.
0 comments:
Post a Comment