Mbeya. Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, imemtimua kazi muuguzi mmoja na mwingine kumshusha madaraja baada ya kugundulika kushiriki vitendo vya rushwa na kunyanyasa wagonjwa.
Wauguzi hao ambao majina yao yanahifadhiwa wanadaiwa kwa kipindi kirefu walikuwa wakituhumiwa kupenda kuomba rushwa kutoka kwa wagonjwa na kwamba pia walionyesha dhahiri kuwanyanyasa walioshindwa kutoa rushwa.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dk Seif Mhina alisema jana kwamba, muuguzi aliyetimuliwa kazi alikuwa chini ya mamlaka ya hospitali yake.
Alisema muuguzi mwingine ni mfanyakazi
wa siku nyingi ambaye ameshushwa vyeo na sasa atakuwa anafyeka majani
na kupalilia maua. Awali ilisemekana, wauguzi hao walilalamikiwa na
wagonjwa na kubainika ni kweli baada ya kuundiwa kamati ambayo ilitimiza
wajibu wake.
Uchunguzi wa kamati ulibaini kuwapo
kwa matukio mengi yaliyowahusisha wauguzi hao na kwamba ndipo hatua za
kinidhamu zilipochukuliwa dhidi yao baada ya kuhojiwa.
Naye Katibu wa Hospitali hiyo, Juliana
Mawalla alisema uongozi hautakubali hospitali hiyo ichafuliwe na
wafanyakazi wachache. CHANZO, MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment