Benki ya dunia imesitisha mkopo wa
dola milioni 90 kwa Uganda wa kuimarisha sekta ya afya kufuatia
kupitishwa kwa sheria inayoharamisha ushoga na kutoa adhabu kali kwa
watakaopatikana na hatia
Hatua hiyo ya benki ya dunia
haikutarajiwa na wengi kwani taasisi hiyo mara nyingi hujiepusha
kuingilia masuala ya ndani ya kisiasa ya nchi wanachama au kuhusiana na
masuala kama haki za mashoga, kuepuka kuzishurutisha nchi wanachame wake
188.
Hata hivyo msemaji wa benki hiyo David
Theis amesema katika barua pepe kuwa wamesitisha mradi huo wa kuboresha
sekta ya afya ya Uganda hadi watakapoufanyia tathmini na kuhakikisha
malengo yake ya maendeleo hayataathiriwa na sheria hiyo mpya ya
kuharamisha ushoga.
Rais wa benki hiyo Jim Yong Kim
amewatumia wafanyakazi wake barua akisema benki ya dunia inapinga
ubaguzi na itawalinda wafanyakazi wake wote na kuongeza kupitishwa kwa
sheria hiyo ya Uganda sio nchi ya kwanza kufanya hivyo kwani ushoga
umeharamishwa katika nchi 83 na zaidi ya nyingine 100 zinawabagua
wanawake.
Mkopo ulikuwa uimarishe sekta ya afya
Licha ya kusimamishwa kwa mkopo huo wa
dola milioni 90,benki ya dunia bado ina miradi mingine nchini Uganda ya
kiasi cha dola bilioni 1.56. Mkopo huo ulitarajiwa kuidhinishwa hapo
jana na ulipaswa kuangazia miradi ya kuboresha afya ya uzazi,afya ya
watoto wachanga na uzazi wa mpango
Kutiwa saini kwa sheria hiyo ya
kuharamisha ushoga Uganda na Rais Yoweri Museveni mapema wiki hii
kumeibua shutuma kali kutoka kwa nchi za magharibi na mashirika ya
kutetea haki za binadamu.
Norway,Denmark na Uholanzi zimetangaza
kuwa zitasitisha misaada kwa serikali ya Uganda kutokana na sheria hiyo
na nchi nyingine wafadhili ikiwemo Marekani pia zimetishia kusitisha
misaada na kutafakari upya uhusiano kati yao na Uganda.
Ghadhabu hiyo ya nchi za magharibi
kuhusu kuharamishwa kwa ushoga ambayo adhabu yake ni kifungo cha maisha
gerezani kwa watakaokutikana na hatia imeporomosha thamani ya shilingi
ya Uganda na kusababisha Benki nchini humo kuingilia kati kwa siku mbili
mfululizo
Kutiwa saini kwa sheria hiyo ya
kuharamisha ushoga Uganda na Rais Yoweri Museveni mapema wiki hii
kumeibua shutuma kali kutoka kwa nchi za magharibi na mashirika ya
kutetea haki za binadamu.
Norway,Denmark na Uholanzi zimetangaza
kuwa zitasitisha misaada kwa serikali ya Uganda kutokana na sheria hiyo
na nchi nyingine wafadhili ikiwemo Marekani pia zimetishia kusitisha
misaada na kutafakari upya uhusiano kati yao na Uganda.
Ghadhabu hiyo ya nchi za magharibi
kuhusu kuharamishwa kwa ushoga ambayo adhabu yake ni kifungo cha maisha
gerezani kwa watakaokutikana na hatia imeporomosha thamani ya shilingi
ya Uganda na kusababisha Benki nchini humo kuingilia kati kwa siku mbili
mfululizo
Serikali ya Uganda haina wasiwasi
Hata hivyo msemaji wa serikali ya
Uganda Ofwono Opondo amesema Uganda inaweza kujiendeleza bila ya misaada
kutoka nchi za magharibi na kuongeza Uganda haina wasiwasi na hatua
hizo kwani ni wakati kwa Afrika kupinga ukoloni, utumwa na ubabe kutoka
magharibi.
Mwanaharakati ambaye amekuwa katika
mstari wa mbele kuwatetea mashoga nchini Uganda Frank Mugisha alikutana
na maafisa wa ngazi ya juu wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani mjini
Washington hapo jana kuomba usaidizi utakaowalinda mashoga.
Ofisi ya kutetea haki za binadamu ya
Umoja wa Mataifa umelaani kuchapishwa kwa majina ya watu wanaodaiwa kuwa
mashoga nchini Uganda katika gazeti moja la udaku nchini humo na kuonya
hatua hiyo inakiuka haki ya kuwa na faragha na kuonyesha wazi kuwa
maisha ya mashoga yamo hatarini.
Kiongozi wa upinzani Uganda Kizza
Besigye ameishutumu serikali kwa kutumia suala hilo kuwahadaa raia wa
nchi hiyo ili wasiangalie masuala muhimu kama ufisadi au kuwepo kwa
jeshi la Uganda Sudan Kusini
0 comments:
Post a Comment