WATU WASIOFAHAMIKA WAFUNGA BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE NA KUPORA MALI ZA ABIRIA WILAYANI MBARALI.
WATU
WASIOFAHAMIKA MAJINA, MAKAZI, WALA IDADI YAO WAKIWA NA SILAHA ZA JADI
MAPANGA, MARUNGU, MAWE NA FIMBO WALIWEKA MAWE MAKUBWA NA MAGOGO KATIKA
BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE NA KUTEKA BAADHI YA MAGARI YALIYOKUWA
YAKIPITA KATIKA BARABARA HIYO. TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE
24.02.2014 MAJIRA YA SAA 01:30HRS USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA MACHIMBO,
KATA NA TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI. KATIKA TUKIO HILO BAADHI
YA ABIRIA WALIPORWA VITU MBALIMBALI IKIWA NI PAMOJA NA PESA TASLIMU,
SIMU ZA MKONONI NA MIKOBA AMBAVYO THAMANI NA IDADI YAKE BADO KUFAHAMIKA.
AIDHA WATU HAO WALIWASHAMBULIA BAADHI YA ABIRIA HAO KWA KUWAPIGA SEHEMU
MBALIMBALI ZA MIILI YAO KWA KUTUMIA SILAHA WALIZOKUWANAZO PIA WALIFANYA
UHARIBIFU KATIKA BAADHI YA MAGARI KWA KUVUNJA VIOO IKIWA NI PAMOJA NA
GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.867 ARX AINA YA TOYOTA NOAH LILILOKUWA
LIKIENDESHWA NA DEREVA AHMED ABDALAH @ AMAN. KATIKA TUKIO HILO MASHAKA
ABDALAH @ CHOMA ALIJERUHIWA NA KULAZWA KATIKA HOSPITALI YA SERIKALI
WILAYA YA MBARALI NA HALI YAKE INAENDELEA VIZURI, WATU WENGINE WAWILI
WALIPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA. HATA HIVYO POLISI WALIOKUWA DORIA
ENEO LA IGAWA MPAKA WA MBEYA NA NJOMBE WALIFIKA MARA MOJA ENEO HILO NA
KUKUTA MAGARI YAKIWEMO YANAYOSAFIRISHWA KWENDA NJE YA NCHI IT YAKIWA
YAMESIMAMISHWA, WATU HAO WALIPOONA GARI LA POLISI WALIKIMBILIA VICHAKANI
NA MAGARI HAYO YALIONDOKA KATIKA ENEO KUENDELEA NA SAFARI. WATU KUMI
[10] WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA MAHOJIANO KUHUSIANA NA TUKIO
HILI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI
ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA WATU WALIOHUSIKA
KATIKA TUKIO HILO AZITOE KWA JESHI LA POLISI/MAMLAKA HUSIKA ILI
WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
MTU
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BARTON MWAKAPINDI [30] MKAZI WA ILEMI
ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA BAADA YA KUKAMATWA AKIWA
NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 2. MTUHUMIWA ALIKAMATWA
KATIKA MSAKO ULIOENDESHWA NA JESHI LA POLISI MNAMO TAREHE 24.02.2014
MAJIRA YA SAA 12:00HRS MCHANA HUKO KATIKA MTAA WA ILEMI, KATA YA ILEMI,
TARAFA YA SISIMBA JIJI NA MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA AMEFIKISHWA
MAHAKAMANI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI
HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU 17 KWA KOSA LA KUNYWA POMBE KABLA YA MUDA.
WATU
17 WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA BAADA YA KUKAMATWA
KWA KOSA LA KUNYWA POMBE KABLA YA MUDA. WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA MNAMO
TAREHE 24.02.2014 MAJIRA YA SAA 12:00HRS MCHANA HUKO KATIKA MTAA WA
MWAFUTE – ILEMI, KATA YA ILEMI, TARAFA YA SISIMBA JIJI NA MKOA WA
MBEYA. WATUHUMIWA WAMEFIKISHWA MAHAKAMANI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI
ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUNYWA POMBE KABLA YA MUDA
ULIOWEKWA NA SERIKALI KWANI KUFANYA HIVYO NI KINYUME CHA SHERIA NA
KAMWE JESHI LA POLISI HALITASITA KUMKAMATA/KUMCHUKULIA HATUA ZA KISHERIA
YEYOTE ATAKAYE KWENDA KINYUME CHA SHERIA. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII
KUTUMIA MUDA HUO KATIKA SHUGHULI ZA KIMAENDELEO NA KUJITAFUTIA KIPATO
KWA NJIA HALALI.
Signed by:
[ROBERT MAYALA – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment