UVUMI
mkubwa umezagaa kwamba kuna tamko litatolewa kwenye Soko la Hisa la New
York linalohusu David Moyes kuondoka Manchester United baada ya Jumanne
Usku kufungwa Bao 2-0 na Olympiacos huko Ugiriki kwenye Mechi ya Kwanza
ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI lakini habari
hizo zimepuuzwa huko Manchester.
Uvumi huo, ambao pia ulikuwepo kwenye
Mitandao ya Kijamii, umeishangaza Klabu ya Manchester ambayo Siku zote
imesisitiza kuwa Meneja wao atapewa muda wa kutosha kujenga Timu yake.
Hilo la kujenga Timu upya lilionekana
wazi kwenye Mechi ya Jana na Olympiacos ambao licha ya kuzidiwa kumiliki
Mpira wao ndio walifunga Bao 2 kupitia Alejandro Dominguez na Joel
Campbell.
Mwenyewe Moyes amekiri uchezaji mbovu wa
Timu yake na amesema: “Huwezi kumchagua hata Mchezaji mmoja ambae
angalau alicheza vizuri. Hatukucheza kabisa!”
Nae Robin van Persie, akiongea na Kituo
cha Habari cha Holland, NOS, alisema: “Inabidi tufanye kazi. Kuna Gemu
nyingie tunacheza vizuri na nyingine hatuchezi vizuri!. Wakati mwingine
tunakosa bahati!”
Licha ya kuongoza kwa Bao mawili ambayo
watatua nayo Old Trafford hapo Machi 19 kwa ajili ya Mechi ya Marudiano,
Mchezaji wa Arsenal, Joel Campbell, ambae yupo kwa Mkopo Olympiacos,
amepuuza hilo na kudai kazi bado ipo.
Campbell, ambae ni Raia wa Costa Rica na
aliejiunga na Arsenal Mwaka 2011 na kutolewa kwa Mkopo, vile vile
amepuuza habari kuwa Bao lake kwenye Mechi hiyo na Man United
litamrudisha Arsenal kwa kusema: “Lile ni Goli muhimu kwangu na
Olympiacos. Siifikirii Arsenal, naijali Olympiacos tu!”
0 comments:
Post a Comment