Kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini.
Kocha wa Manchester City Manuel
Pellegrini amepigwa marufuku mechi mbili na UEFA asisogelee eneo la
kiufundi la uwanja kwa kumlaumu mwaamuzi baada ya klabu yake kushindwa
na Barcelona katika michuano ya klabu bingwa ya Ulaya.
Pellegrini alisema baada ya timu yake
kushindwa 2-0 nyumbani kwamba mwaamuzi kutoka Sweden Jonas Eriksson
"hakua mwaadilifu kwa timu zote mbili".
Alituhumiwa kwa ukosefu wa nidhamu na
amepewa adhabu ya kukaa jukwaani pamoja na mashabiki katika mkondo wa
pili wa mchuano na Barcelona mnamo Machi 12 March, poja na Mechi
nyingine za ziada.
Adhabu ya mechi moja nyingine imesimamishwa kwa miaka miwili.
Chanzo, bbcswahili
0 comments:
Post a Comment