Sunday, 23 February 2014

MVUA YASABABISHA HASARA YA MILIONI 400 HALMASHAURI YA ARUSHA

index 
Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Vijijini imepata hasara ya zaidi ya milioni 400 kutokana na mvua zilizonyesha kwa kipindi cha mwaka jana ambapo mvua hizo ziliharibu vibaya baadhi ya miundombinu ya Halmashauri hiyo
Akiongea na “FULLSHANGWE” mapema leo Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo ambaye ni Bw Fidelis Lumato alisema kuwa uharibifu huo ulitokana na mvua kubwa ambazo zilinyesha mwaka jana na hivyo kusababisha madhara makubwa

Lumato alisema kuwa mvua hizo zilikuwa zinatokea katika mlima wa Meru ambazo pia zilikuja kama mafuriko na kisha kuharibu hata miundo mbinu kama vile madaraja jambo ambalo kwa sasa limebaki kama changamoto kubwa sana katika Halmashauri hiyo
Alidai kuwa maji ya mvua ambayo yalikuwa yanatoka katika Mlima wa Meru yalikuwa yanakuja moja kwa moja kwenye Miundo mbinu ya Halmashauri hiyo jambo ambalo lilifanya baadhi ya wananchi kuwa kwenye wakati mgumu kutokana na wengi wao kutegemea miundo mbinu hiyo kama kivukio

Alidai kuwa kutokana na kuwa wameweza kupata hasara hiyo ya kiasi cha zaidi ya Milioni 400 mpaka sasa wameshaweza kuweka utaratibu mbalimbali wa kuweza kusaidia wananchi ili hata wakati wa mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha kwa msimu wa mwaka huu basi zisiweze kusababisha madhara makubwa sana.

Alitaja utaratibu huo kuwa ni pamoja na kuweza kujenga na kukarabati madaraja ambapo yataweza kusaidia maji au mafuriko yatakayotokea Mlima meru yasiweze kuwa na madhara kwa wananchi wa Halmashauri ya Arusha Vijijini.

“hapa tunachangamoto kubwa sana ya ukosefu wa madaraja ambayo yaliharibika kutokana na mvua zilizonyesha mwaka jana na mpaka sasa kama nilivyosema ni kuwa tayari tumepata hasara ya Milioni 400 na pia mpaka sasa tuna mikakati mbalimbali ya kuweza kuwasaidia wanancfhi wasiweze kupata madhara zaidi hasa nyakati hizi za mvua”aliongeza Lumato


wakati huo huo aliwatwaka wananchi nao kuhakikisha kuwa wanalinda na kuhifadhi rasilimali za umma kama vile Miundombinu kwani pia napo miundombinu inapoharibiwa inachangia sana Halmashauri kuendelea kupata hasara.

0 comments: