-Kufanyika Septemba 22 hadi 28
-Vikundi zaidi ya 40 vinatarajiwa kutoa burudani
-wadau na wadhamini milango ipo wazi sasa
Na Andrew Chale, Bagamoyo
TAMASHA
la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo ambalo kwa mwaka huu (2014)
litakuwa la 33, ambapo linatarajia kulindima kwa siku saba, kuanzia
Septemba 22 hadi 28, kwenye viunga vya Chuo cha Sanaa Bagamoyo.
Tamasha
hilo la 33, mwaka huu, lenye kauli mbiu, “Sanaa na Utamaduni katika
kukuza Utalii”, limekuwa msaada mkubwa kwa wasanii na vikundi mbali
mbali kujitangaza kitaifa na kimataifa pamoja na kutoa fursa za
kibishara katika kipindi chote cha tamasha.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Tamasha hilo, Abraham Bafadhil ‘Bura’, alieleza
kuwa, tayari mipango na maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea katika
kufikia malengo huku akiwaomba wadau kujitoakeza na kudhamini tamasha
hilo.
Moja ya mchezo wa igizo la hisia kali, lililofanywa na walimu wa chu cha sanaa Bagamoyo 2013.
“Milango
ipo wazi hivyo, kwa wadhamini kujitokeza na kuchangamkia fursa hii
hadimu, kwani tamasha hili ni kongwe katika ukanda huu wa Afrika ya
Mashariki na Afrika kwa ujumla” alisema Bura.
Na
kuongeza kuwa, tamasha hilo lenye mvuto wa kipekee ndani na nje ya
Tanzania, limekuwa likipata umaarufu mkubwa kila mwaka kutokana na idadi
kubwa ya watazamji wa ndani na wale wa kutoka Mataifa mbali mbali
duniani.
Kwa
upande wake, Katibu wa tamasha hilo, Benjamini Mahimbali alieleza kuwa,
tamasha hilo limekuwa na mafanikio ikiwemo ongezeko kubwa la watazamaji
na vikundi vinavyoomba kufanya maonyesho.
“Idadi
ya watazamaji na imekuwa ikiongezeka kila mwaka, huku kwa mwaka jana
tulikuwa na wastani wa watazamaji elfu nne mia saba kwa siku (4,700),
ikiwemo wa rika zote.” Alisema Ben.
Na
kuongeza kuwa, wanatarajia ongezeko hilo kuwa kubwa zaidi kutokana na
maboresho na mipango mbali mbali inayotarajiwa kufanyika mwaka huu.
Moja ya vikundi vya kigeni kutoka Norway kikiwajibika jukwaani 2012.
Katika
tamasha hilo maonyesho mbali mbali yanatarajiwa kuonyeshwa ikiwemo;
Muziki wa aina tofauti, ngoma, maigizo, sarakasi, mazingaombwe na
maonyesho kemkem ya sanaa na utamaduni wa Mtanzania na ya Mataifa
mengine duniani.
Kwa
upande wa fomu za kushiriki tamasha hilo ambalo kwa mwaka huu
wanatarajia kupokea vikundi zaidi ya 40, zinatarajiwa kutolewa kwenye
ofisi za Chuo hicho pamoja na tovuti ya chuo (www.tasuba.ac.tz)
Baadhi ya watazamaji wakifuatilia moja ya maonyesho ya tamasha hilo.
Au Kwa mawasiliano na maulizo juu ya ushiriki na udhamini waweza kufika Chuo cha Sanaa Bagamoyo (TaSUBa) au kupitia namba;
0 comments:
Post a Comment