Sunday, 23 February 2014

NCHI YA UKRAINE YAPATA RAIS WA MUDA

 
Rais wa muda wa Ukraine Oleksander Turchinov

Bunge la Ukraine limemteua spika kuwa rais wa muda, siku moja baada ya kupiga kura kumtoa madarakani Rais Viktor Yanukovich kufuatia maandamano makubwa.
Spika, Oleksander Turchinov, aliwasihi wabunge wakubaliane juu ya serikali ya umoja wa taifa ifikapo Jumaane.
Yeye ni mshirika mkubwa wa waziri mkuu wa zamani, Yulia Tymoshenko, ambaye alifunguliwa kutoka gerezani Jumamosi.
Chama cha Yanukovych kinasema wa kulaumiwa kwa ghasia zilizotokea Kiev na kuuwa zaidi ya watu 80, ni Bwana Yanukovych mwenyewe na watu walio karibu naye.
Rais huyo aliyeng'olewa amekimbia kutoka mji mkuu na amri imetolewa kuwa maafisa wakuu wa zamani wakamatwe kwa mauaji hayo.
Maelfu ya watu bado wako katika medani ya Uhuru, chimbuko la maandamano.

0 comments: