Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
leo, Ijumaa, Februari 28, 2014 hatahutubia taifa katika hotuba yake ya
mwisho wa mwezi kama ilivyo kawaida.
Hotuba
hiyo haitakuwepo kwa sababu awali Rais Kikwete alitarajiwa kuzindua
Bunge Maalum la Katiba kwa hotuba rasmi Bungeni mjini Dodoma leo kabla
ya ratiba ya shughuli za Bunge hili kufanyiwa mabadiliko. Rais Kikwete
sasa atalizindua Bunge hilo wiki ijayo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment