£30,000 - Wastani wa mshahara wa wiki
kwa mchezaji wa ligi kuu ya England, hii ni kwa mujibu wa Deloitte's
sports business group.
£517 - Huu ni wastani wa mshahara wa
wiki wa mtu anayefanya kazi ndani ya UK. Waziri mkuu wa Uingereza David
Cameron anapata £2,740 kila wiki.
65 - Itamchukua wiki 65 kwa Barack
Obama, raisi wa taifa kubwa duniani Marekani, kuweza kutengeneza kiasi
anacholipwa Rooney ndani ya siku saba tu - Obama analipwa £240,000 kwa
mwaka.
1885 - Huu ulikuwa mwaka wa kwanza kwa mwanasoka kuweza kulipwa kutokana na kucheza soka.
£4 - Hiki ndio kilikuwa kiwango cha juu kabisa cha malipo katika Football League mwaka 1901.
£4 - Hiki ndio kilikuwa kiwango cha juu kabisa cha malipo katika Football League mwaka 1901.
60 - Namba ya miaka iliyotumika mpaka
kufikia mwisho wa sheria ya kulipwa kiasi kisichozidi paundi 4 kwa
mwanasoka. Sheria hii ilikufa mwaka 1961. Muda mfupi baada ya kufutwa
kwa sheria hii, mchezaji wa Fulham na Engand Johnny Haynes alikuwa
mchezaji wa kwanza kulipwa kiasi cha £100 kwa wiki.
£1,200 - Kiasi ambacho golikipa Peter
Shilton alitengeneza kila wiki mwaka 1979 wakati alipoweka rekodi ya
kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi zaidi Uingereza kwa kusaini
mkataba mpya na Nottingham Forest.
£10,000 - Mchezaji wa kwanza kulipwa
kiasi cha tarakimu 5 alikuwa Chris Sutton, wakati mshambuliaji huyo
alipojiunga na Blackburn Rovers akitokea Norwich City mnamo 1994.
£100,000 - Sol Campbell aliondoka
Tottenham na kujiunga na Arsenal mnamo mwaka 2001, akasaini mkataba
ambao ulimfanya kuwa muingereza wa kwanza kulipwa mshahara wenye
tarakimu 6 kila wiki. Chanzo: shaffihdauda
0 comments:
Post a Comment