MABINGWA
WA TANZANIA BARA, Yanga, Leo hii wanatinga Uwanja wa Taifa Jijini Dar
es Salaam kuwavaa Mabingwa wa Afrika, Al Ahly, katika Mechi ya Kwanza ya
Raundi ya Kwanza ya CAF CHAMPIONZ LIGI.
Timu hizi zitarudiana huko Cairo, Misri hapo Machi 9.
Wakati Al Ahly ikiwania kutwaa Ubingwa
wao wa 3 mfululizo wa Afrika na ambao utakuwa Ubingwa wao 9, Yanga bado
hawajaambua kitu kwenye michuano hii mikubwa Barani Afrika.
Wakati Yanga ipo Nafasi ya Pili kwenye
VPL, Ligi Kuu Vodacom, na imepitwa tu na Azam FC kwa vile wamecheza
Mechi moja zaidi, Al Ahly, wanaotetea Ubingwa wao wa Misri waliotwaa
Mwaka 2011 kwani 2012 Ligi haikuchezwa huko Misri kutokana na vurugu,
Msimu huu wapo Nafasi ya 4 baada kufungwa Mechi 3 katika Mechi 9 za
Ligi.
Ingawa Al Ahly ni miamba wa kweli wa
Afrika, Kihistoria mbinu zao za kucheza Ugenini ni kujihami na
kuhakikisha hawafungwi ili ‘waue’ huko Cairo.
Hivyo Mechi hii ya Leo ni wazi mzigo
mkubwa utakuwa kwa Washambuliaji wa Yanga wakiongozwa na Supastraika
Mrisho Ngassa, ambae alipiga Hetitriki mbili katika Mechi mbili za
Raundi iliyopitwa walipoitwanga Komorozine ya Comoro Jumla ya Bao 12-2,
pamoja na wenzake Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza na Emmanuel Okwi.
Ngome ya Al Ahly, chini ya Mkongwe Wael
Gomaa, ni imara na wana Wachezaji hatari kina Gedo na Emad Meteb lakini
safari hii watamkosa Gwiji Mohammed AbouTrika ambae amestaafu.
VIKOSI VINAWEZA KUWA:
YANGA: Juma Kaseja,
Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Frank Domayo,
Saimon Msuva, Mrisho Ngasa, Didier Kavumbagu, Emmanuel Okwi, Hamis
Kizza
AL AHLY: Sherif Ekramy, R. Rabia, S. Samir, Wael Goma, S. Moawad, H. Ashour, S. Ahmed, A. Saied, A. Shoukri, R. Sobhi, A. Raouf
REFA: Haileyesus BAZEZEW BAZEZEW BELETE [Ethiopia]
CAF CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Kwanza
Jumamosi Machi 1
Dynamos – Zimbabwe v AS Vita Club - Congo, DR
Young Africans – Tanzania v Al Ahly - Egypt
AC Leopards de Dolisie – Congo v Primeiro de Agosto - Angola
Flambeau de l’Est – Burundi v Coton Sport FC - Cameroon
Nkana FC – Zambia v Kampala City Council FC - Uganda
Gor Mahia – Kenya v Espérance Sportive de Tunis - Tunisia
Al Zamalek – Egypt v Kabuscorp - Angola
Kaizer Chiefs - South Africa v Liga Muculmana de Maputo – Mozambique
Stade Malien de Bamako – Mali v Al-Hilal - Sudan
Jumamosi Machi 2
Enyimba International FC – Nigeria v AS Bamako - Mali
Entente Sportive de Sétif - Algeria v ASFA-Yennenga - Burkina Faso
Berekum Chelsea – Ghana v Al Ahli - Benghazi - Libya
Les Astres de Douala - Cameroon v TP Mazembe - Congo, DR
The Barrack Y.C.II – Liberia v Sewe Sport - Ivory Coast
Horoya Athlétique Club – Guinea v Raja Club Athletic - Morocco
0 comments:
Post a Comment