Rais Barack Obama akizungumzia kuhusu hali nchini Ukraine.
Marekani imeonya kuwa rais Barack
Obama pamoja na viongozi wengine wa Ulaya wataususia mkutano wa kundi la
mataifa ya G8 mjini Sochi iwapo wataona kuwa Urusi inaingilia uhuru wa
Ukraine.
Obama ameeleza wasi wasi wake mkubwa
kuhusiana na ripoti kuwa majeshi ya Urusi yameingia mjini Crimea,
kufuatia madai yaliyotolewa na afisa wa serikali mjini Kiev kuwa uvamizi
umeanza.
Maafisa waandamizi wamesema rais
ameamua kujitokeza katika ikulu ya Marekani ya White Housena kutoa
maelezo baada ya nchi hiyo kuamua kuwa kulikuwa na ushahidi kwamba
majeshi ya Urusi ni kweli yako ndani ya Ukraine.
Vikosi vyenye silaha nzito na katika
sare ambazo hazina nembo ya taifa vimeonekana kuzunguka majengo ya
serikali na katika uwanja wa ndege katika mji wa Crimea wa Simferopol ,
wakati maafisa wa Ukraine wakiishutumu Urusi kwa kile walichokiita
uvamizi wa wazi.
Majeshi ya Urusi
Mzozo huo ulianzia katika mzozo wa
kisiasa na kiuchumi kufuatia kuondolewa kwa serikali inayoelemea upande
wa Urusi mjini Kiev na kuingia katika mpambano wa kieneo baada ya madai
ya maafisa wa Ukraine kuwa kiasi ya wanajeshi 2,000 wa Urusi wamewasili
mjini Crimea.
"Tuna wasi wasi mkubwa sasa kuhusiana
na ripoti za harakati za kijeshi zinazochukuliwa na shirikisho la Urusi
ndani ya Ukraine," Obama amesema.
Afisa wa jeshi ameliambia shirika la
habari la AFP baada ya taarifa ya rais kwamba " inaonekana kama
wameingiza wanajeshi kadha nchini humo.
Afisa huyo amesema kuwa Urusi haijatoa
tahadhari yoyote kabla kuhusu harakati hizo. Obama anatambua kuwa Urusi
imekuwa na maslahi yake pamoja na uhusiano wa kiutamjaduni na kiuchumi
na Ukraine, na imekuwa na maeneo ya kijeshi katika eneo la Crimea, eneo
ambalo liliunganishwa na jamhuri ya zamani ya Kisoviet ya Ukraine katika
umoja wa Kisoviet mwaka 1954.
Obama aonya
Lakini amesema ukiukaji wowote wa
uhuru wa Ukraine pamoja na ardhi ya nchi hiyo utaiyumbisha kwa kiasi
kikubwa Ukraine. "Marekani itasimama pamoja na jumuiya ya kimataifa
katika kusisitiza kuwa kutakuwa na gharama katika uvamizi wowote wa
kijeshi nchini Ukraine," alisema rais Obama.
Afisa mwingine mwandamizi baadaye
amedokeza kuwa gharama hizo zinaweza kujumuisha uamuzi wa Obama na
viongozi wengine wa ngazi ya juu wa Ulaya kususia mkutano wa nchi zenye
utajiri mkubwa wa viwanda za G8 mkutano utakaofanyika katika mji wa
kitalii uliofanyika michezo ya Olimpiki wa Sochi mwezi Juni.
Uwezekano mwingine wa kibiashara na
kiuchumi ambao Urusi ilikuwa inataka hadi wiki hii huenda ukaingia
katika hali shaka , afisa huyo amesema.
Urusi pia itavuruga nafasi yake ya
kuonekana kuwa na mvuto duniani baada ya michezo ya majira ya baridi,
ambayo ilimalizika mwishoni mwa juma lililopita, ameeleza afisa wa
Marekani.
Chanzo, dw.de/swahili
0 comments:
Post a Comment