Mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mwashinga Mlozi, akizungumza na madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Singida.Pamoja na mambo mengine, aliagiza kwamba Diwani na mtendaji wake wa kata wasipomaliza ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara kabla ya Mei 30 mwaka huu, atawachukulia hatua kali ya kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani. Wa pili kulia (aliyeketi),ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Singida,Illuminata Mwenda na anayefuata ni mwenyekiti wa halmashauri ya Singida.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida.
MKUU
wa wilaya ya Singida,Queen Mwashinga Mlozi,amewatahadharisha madiwani
na watendaji kata,kwamba kabla ya mei 30 mwaka huu wawe wamekamilisha
ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara,vinginevyo watachukuliwa hatua kali
za kisheria.
Mlozi ametoa agizo hilo wakati akizungumza mbele ya kikao cha kawaida cha baraza la madiwani kilichofanyika mjini Singida.
Alisema
madiwani na watendaji kata ambao watashindwa kumaliza ujenzi huo kabla
ya muda uliopangwa,watawajibishwa ikiwa ni pamoja na kuwafikisha
mahakamani.
“Nitafanya
hivyo kwa mujibu wa mamlaka niliyopewa chini ya kifungu cha 14 na 15
vya sheria za tawala za mikoa na serikali za mitaa ya mwaka 2002 ya
kuvunja amri halali ya kutokujenga vyumba vitatu vya maabara”alifafanu
mkuu huo wa wilaya.
Dc
Mlozi alitaja shule za kata ambazo ujenzi wake umefikia asilimia
80,kuwa ni
Mdasenga,Maghojoa,Ntoge,Mughunga,Makuro,Mrama,Mwanamwema,Ngimu,Nyeri na
Itaja.
Katika
hatua nyingine,alisema kuwa kampuni ya bia Tanzania (TBL) kwa
kushirikiana na taasisi za fedha,imeazimia kufanya zao la mtama
(mweupe),kuwa zao la kutumainiwa la biashara katika mkoa wa Singida.
Akifafanua,Mlozi
alisema TBL inahitaji kununua tani 7,000 na ili kufikia lengo la
upatikanaji wa tani hizo,taasisi za fedha za CRDB benki na
NMB,zitashirikiana na wakulima ili kuhakikisha wanalima kitaalam kwa
kutumia zana bora na kilimo cha kisasa.
“Madiwani
na watendaji wote tutumie fursa hii kwa kuhakikisha tunawahamasisha
wakulima wetu wanufaike na kilimo hiki cha mtama mweupe.Tujipange vizuri
kwa utekelezaji”,alisema Mlozi.
0 comments:
Post a Comment