Sophia Kindamba akiwa na mwanae Junior Richard Rutta ..................................... |
MTOTO
Junior Richard Rutta ambaye jinsi yake haieleweki anatafuta msaada
utakaomuwezesha kufanyiwa uchunguzi katika hospitali ya CCBRT, jijini
Dar es Salaam.
Mtoto huyo mwenye miaka miwili na miezi saba anaishi na mama yake mzazi, Sophia Kindamba, mtaa wa Mtwivilla, mjini Iringa.
Akiomba
msaada huo, mama yake alisema jitihada za madaktari wa hospitali ya
Taifa ya Muhimbili kuchunguza na hatimaye kujua mtoto huyo ana jinsi
gani zinaelekea kukwama.
“Kwa
mara ya kwanza nilimpeleka katika hospitali hiyo mwanzoni mwa mwaka
2012, lakini hadi hii leo hakuna majibu yoyote; kwahiyo haieleweki kama
ni msichana au ni mvulana” alisema huku machozi yakimtoka.
Alisema
mapema mwaka huu alikwenda Muhimbili lakini kwa majibu aliyopewa
amepoteza imani ya tatizo la mwanae kushughulikiwa hospitalini hapo.
Kindamba
alisema “nimeambiwa kipimo kile kinatakiwa kupelekwa nje ya nchi baada
ya uchunguzi wake hospitalini hapo kushindikana.”
Alisema wakati akipewa majibu hayo ameshauriwa akajaribu pia kupata vipimo hivyo katika hospitali ya CCBRT.
“Nimerudi Iringa kutafuta hela ili nikienda CCRBT nisipate shida ya gharama za uchunguzi na matibabu,” alisema.
Kindamba
alisema Katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa leo amempa barua
itakayomuwezesha kupita kwa watu, taasisi na mashirika mbalimbali kuomba
mchango.
“Naomba
mnichangie; baba wa mtoto alinikimbi baada ya kubaini mtoto ana tatizo
hili na sijui aliko; mimi mwenyewe nashindwa kufanya biashara yangu ya
kutembeza mitumba kwasababu hali ya mtoto huyu sio nzuri,” alisema.
Alisema
mtoto huyo huanguka na kupoteza fahamu kwasababu ana tatizo lingine la
mtindio wa ubungo lililogundulika katika hospitali ya Muhimbili.
ASante
kwa kutembelea blog yetu ya mbeyagreennews MUNGU
AKUBALIKI (GOD BLESS)
0 comments:
Post a Comment