Basi Ripoti mpya kutoka benki ya dunia inasema kuwa robo ya chakula chote kinachokuzwa duniani hupotea ama kutupwa, na sasa inawataka raia kufikiri kwa makini kile kuhusu uharibifu huu wa chakula.
Inasema kuwa katika maeneo kama vile Marekani na Uchina ,watumiaji wa chakula ndio wa kulaumiwa pakubwa kwa kupoteza chakula hicho.
Lakini katika jangwa la Sahara chakula kingi hupotea wakati wa uzalishaji.
Benki ya dunia inasema kuwa kati ya asilimia 25 na 35 ya chakula chote kinachokuzwa duniani hutupwa.
katika mataifa yanye utajiri wa
viwanda ,lawama kubwa zaidi huwaendea watumiaji wa chakula hicho ambao
hukiwacha chakula kuoza katika jokovu.
Raia wa marekani kazkazini ni miongoni
mwa wale walio na lawama kubwa kwa kuwa asilimia 61 ya chakula chao
huharibika wakati wa matumizi.
Mwandishi wa ripoti hiyo Jose Cuesta anasema kuwa kile kinachohitajika ni kubadili tamaduni.
Lakini katika jangwa la Sahara chakula kingi huharibika wakati wa uzalishaji .
Benki kuu duniani inasema kuwa kiwango
cha chakula kinachotupwa kinaweza kutofautisha kati ya chakula bora na
uhaba wa chakula katika mataifa mengi.
Imeonya kuwa iwapo mbinu za uzalishaji
hazitaimarishwa na tabia za kula kubadilishwa ,dunia huenda ikakumbwa
na uhaba wa chakula kwa idadi kuu ya watu inayozidi kuongezeka.
Chanzo, bbcswahili
0 comments:
Post a Comment