Alikuwa
kwenye ziara katika shule za sekondari za wilaya hiyo mpya, ambapo
kwanza aligundua wanafunzi wengi hawajaripoti shuleni kuanza Kidato cha
Kwanza.
Toima
alipohoji kulikoni hawajaripoti katika shule walizopangiwa huku wale
walioandikishwa darasa la kwanza, pia nao hawaripoti, alielezwa kuwa
sababu za kiimani zinazokataza wengine kusoma.
Mkuu huyo
wa Wilaya alikatiza ziara yake na kuanza msako wa kuwasaka wanafunzi
hao ambao hawajaripoti shuleni pamoja na waumini wa dini hiyo ya
Matengenezo.
Alisema
aliamua kufanya hivyo, kwa sababu dini hiyo inawakosesha watoto haki yao
ya msingi na kukiuka sheria za nchi, kwani ni haki ya kila mtoto kupata
elimu.
Katika
msako huo, aliongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo na
watendaji wa Halmashauri wakiwemo Maofisa Elimu Msingi na Sekondari.
Viongozi
hao walifika katika familia ya Mchungaji wa Kanisa la Matengenezo, Medad
Laurent (40). Baada ya kufika hapo, Toima aliwakuta mabinti watatu
waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza mwaka huu lakini
hawajaenda, kutokana na kile Mchungaji huyo alichodai kuwa sekondari
wanafundisha uongo, kinyume na maandiko matakatifu yanavyosema.
Kutokana
na hali hiyo, Mkuu wa Wilaya aliamuru Mchungaji huyo na mabinti zake
wawili, kushikiliwa na Jeshi la Polisi huku utaratibu wa kuwapeleka
mabinti hao shule ukiendelea. Pia, aliamuru Mchungaji huyo kuchukuliwa
hatua kali kwa mujibu wa sheria za elimu.
Siku
iliyofuata Toima na Kamati ya Ulinzi na Usalama, walifanya kikao na
kukubaliana kuwapeleka mabinti hao, Naomi Medard (16) na Anastazia
Medard (14) katika shule za sekondari zenye mabweni kwa kuwatenganisha
ili wasiendelee kusambaza sumu ya kukataa shule.
Naomi
alipelekwa Shule ya Sekondari Nyamtukuza na Anastazia Shule ya Sekondari
Kanyonza. Hata hivyo, katika familia hiyo binti mmoja Beatrice Merdad
(19) alibaki nyumbani kwa madai kuwa hakuchaguliwa kuendelea na Kidato
cha Kwanza.
Alidai
kuwa hata angechaguliwa, asingeweza kuendelea kwani wanafundisha uongo
na siku akifa hatakuwa na la kwenda kumwambia Muumba wake, kutokana na
elimu hiyo ya dunia kuwapotosha.
Katika
familia hiyo ya watoto saba, wawili walifariki dunia kutokana na
kutokwenda hospitali. Mama wa watoto hao, Julitha Sebastian (39)
alipohojiwa baada ya mtoto wake mchanga kuonekana kudhoofika na nywele
kubadilika rangi, alisema kuwa dini yao haiwaruhusu kwenda hospitali.
Alisema
hakuwahi kumpatia mtoto huyo chanjo ya aina yoyote wala hakuwahi
kujifungulia hospitali. Kuhusu watoto wake waliokufa, alisema Biblia
inasema “Ni heri wafao katika Bwana”.
Kaimu
Ofisa Elimu Sekondari wa Wilaya hiyo, Florida Gandye alisema waumini wa
kanisa hilo, awali walikuwa Wakristo Wasabato, kisha wakajiengua na
kuanzisha dini hiyo yenye imani za ajabu.
CHANZO:HABARILEO
0 comments:
Post a Comment