ANOETA
ni Uwanja ambao FC Barcelona walikuwa hawajashinda katika Mechi zao 5
zilizopita na Jana Usiku walipata kipondo cha Bao 3-1 kutoka kwa Real
Sociedad katika Mechi ya La Liga na kuwabakisha Real Madrid wakiwa
kileleni mwa Ligi hii ya Spain.
Barca, wakitokea kwenye furaha ya
kuichapa Manchester City 2-0 huko Etihad katika Mechi ya UEFA CHAMPIONZ
LIGI Jumanne iliyopita, walijikuta wako nyuma kwa Bao 1 katika Dakika ya
32 kupitia kichwa cha Gorka Elustondo kilichomgonga Begani Alex Song na
kutinga.
Dakika 4 baadae Lionel Messi
akaisawazishia Barca lakini Bao 2 za Real Sociedad ndani ya Dakika 14 za
kwanza za Kipindi cha Pili zilizofungwa na Antoine Griezmann na David
Zurutuza, zilihakikisha Barca wanaondoka Uwanjani Anoeta, Mjini San
Sebastian mikono mitupu kwa mara ya 3 katika Misimu minne.
Pia Mapema Jana, Real Madrid, ikicheza bila ya Cristiano Ronaldo aliekuwa akimalizia Kifungo chake cha Mechi 3, iliichapa Elche Bao 3-0 kwa Bao za to Asier Illaramendi, Gareth Bale na Isco, na kutwaa uongozi wa La Liga wakiwa Pointi 3 mbele ya Barca na Atletico Madrid.
Leo, Atletico Madrid wanacheza Ugenini na Osasuna na wakishinda Bao 4-0 watatwaa uongozi wa Ligi.
MSIMAMO-Timu za Juu:
NA | TIMU | P | W | D | L | F | A | GD | PTS |
1 | Real Madrid CF | 25 | 20 | 3 | 2 | 70 | 24 | 46 | 63 |
2 | FC Barcelona | 25 | 19 | 3 | 3 | 70 | 20 | 50 | 60 |
3 | Atletico Madrid | 24 | 19 | 3 | 2 | 59 | 16 | 43 | 60 |
4 | Athletic de Bilbao | 24 | 13 | 5 | 6 | 43 | 30 | 13 | 44 |
+++++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA/MATOKEO:
Ijumaa Februari 21
Real Valladolid 1 Levante 1
Jumamosi Februari 22
Real Madrid CF 3 Elche CF 0
Celta de Vigo 1 Getafe CF 1
Real Sociedad 3 FC Barcelona 1
UD Almeria 0 Malaga CF 0
Jumapili Februari 23
[Saa za Bongo]
1400 Rayo Vallecano v Sevilla FC
1900 Real Betis v Athletic de Bilbao
2100 Valencia v Granada CF
2300 Osasuna v Atletico de Madrid
2359 RCD Espanyol v Villarreal CF
0 comments:
Post a Comment