>>YANGA v AL AHLY: MAANDALIZI YAKAMILIKA!
>>VPL: MAREKEBISHO-PRISON, SIMBA KUCHEZA MACHI 9!
>>TFF KUADHIMISHA MIAKA 50 KUJIUNGA FIFA, YAUNDA KAMATI!!
SOMA ZAIDI:
Release No. 035
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Februari 28, 2014
MALINZI AUNDA KAMATI YA MIAKA 50 FIFA
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameunda kamati ya watu tisa kuratibu
maadhimisho ya miaka 50 tangu TFF ilipojiunga na Shirikisho la Kimataifa
la Mpira wa Miguu (FIFA).
TFF ilipata uanachama wa shirikisho hilo
la kimataifa Oktoba 8, 1964 ambapo itaadhimisha miaka hiyo 50 kwa
kufanya shughuli mbalimbali za mpira wa miguu.
Kamati hiyo itaongozwa na Mhariri
Mtendaji wa kampuni ya magazeti ya Serikali, Gabriel Nderumaki wakati
Katibu atakuwa Lina Kessy ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF
na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Wanawake (TWFA).
Wajumbe ni Ahmed Mgoyi, Hoyce Temu,
Teddy Mapunda, Ruge Mutahaba, Richard Kasesela, Boniface Wambura na
Meneja Biashara wa TFF anayetarajiwa kuajiriwa hivi karibuni.
Kamati itafanya kikao chake cha kwanza
Jumatatu (Machi 3 mwaka huu) kwenye hoteli ya Courtyard iliyopo Upanda
Seaview saa 7 mchana.
KILA LA KHERI YANGA MECHI YA LIGI YA MABINGWA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) linaitakia kila la kheri yake kwenye mechi yake ya kwanza ya
raundi ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly kutoka
Misri.
Mechi hiyo inachezwa kesho (Machi 1
mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia 10 kamili jioni. Timu
hizo zitarudiana Machi 9 mwaka huu jijini Cairo, Misri.
Maandalizi ya mechi hiyo yamekamilika
ambapo kamishna Abbas Sendyowa kutoka Uganda na waamuzi wanne kutoka
Burundi tayari wapo nchini kwa ajili ya mechi hiyo inayotarajiwa kuvuta
maelfu ya washabiki.
Milango yote katika uwanja huo itakuwa
wazi, ukiwemo ule wa upande wa Uwanja wa Ndani (Indoor Stadium) wakati
Barabara ya Taifa (Taifa Road) itafungwa kuanzia chuo cha DUCE hadi
msikitini kuanzia saa 4 asubuhi.
Magari maalumu yenye sticker pekee ndiyo
yatakayoruhusiwa kuingia uwanjani. Vilevile washabiki wanakumbushwa
kuwa hawaruhusiwi kuingia uwanjani wakiwa na silaha au vifaa vyovyote
vya chuma.
MAREKEBISHO YA MECHI VPL, FDL
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB)
imefanya marekebisho madogo ya ratiba kwa mechi mbili za Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL) na moja ya Ligi Daraja la Kwanza (VPL).
Mechi namba 143 kati ya Tanzania Prisons
na Simba iliyokuwa ichezwe Machi 8 mwaka huu sasa imesogezwa kwa siku
moja hadi Machi 9 mwaka huu, kwa vile Machi 8 mwaka huu Mbeya City
itautumia uwanja huo kwa mechi nyingine ya VPL.
Nayo Mgambo Shooting iliyokuwa icheze na
Kagera Sugar, Aprili 12 mwaka huu Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga sasa
imesogezwa hadi Aprili 13 mwaka huu kwa vile Kituo cha Tanga kitakuwa
na mechi mbili.
Kwa upande wa FDL, mechi ya Mkamba
Rangers na Kimondo SC sasa itachezwa Machi 3 mwaka huu badala ya Machi 9
mwaka huu mjini Ifakara. Mechi hiyo imerudishwa nyuma ili kuipunguzia
gharama Kimondo SC kwani Machi 1 mwaka huu itacheza na Burkina Faso
mjini Morogoro.
Boniface Wambura Mgoyo
Media and Communications Officer
Tanzania Football Federation (TFF)
0 comments:
Post a Comment