Na Datus Boniface, Jeshi la Polisi
JESHI
la Polisi mkoa wa Iringa limepiga marufuku kwa Mwananchi kuhudhuria
mikutano ya kampeni wakiwa na marungu na mapanga hasa wakati huu wa
kampeni za kuwania kiti cha Ubunge Jimbo la Kalenga.
Aidha,
limewataka kuacha mara moja wataka wamiliki wa Malori kubeba wafuasi na
wapenzi wa vyama vya siasa kwa lengo la kuwapeleka katika mikutano ya
kampeni.
Akizungumza
jana na waandishi wa habari, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa
Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Peter Kakamba alisema Jeshi la
Polisi halitavumilia mtu atakayevunja sheria katika kipindi hiki cha
Kampeni na uchaguzi.
“Uzoefu
tuliopata katika chaguzi ndogo za Udiwani wa Kata za Nduli, Ibumu na
Ukumbi ziligubikwa na vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani ikiwemo
wafuasi wa vyama mbalimbali kushambuliana pamoja na kutembea na marungu
na mapanga”alisema
Aliongeza
kwamba, katika chaguzi hizo yalitokea matukio mbalimbali yakiwemo ya
kuingiliana ratiba za kampeni na viwanja na pia kujichukulia sheria
mkononi kwa kuwapiga watu bila sababu za msingi au kwa hisia kwamba ni
wapinzani wa vyama vyao.
Kaimu
Kamanda alisema, tayari kampeni za uchaguzi katika Jimbo la Kalenga
zimeshaanza tangu Februali 19 na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA),kimezindua kampeni zake Februali 22 kwa Kata ya Kalenga.
Alisema
Jeshi la Polisi limejipanga vizuri kuhakikisha kampeni hizo zinafanyika
kwa amani na utulivu ambapo pia Polisi watasimamia vizuri ulinzi siku
ya uchaguzi hadi kutangazwa kwa matokeo.
Hivyo,
aliwataka viongozi wa vyama vya siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi
huo pamoja na wafuasi wao kufanya kampeni za kistaarabu bila fujo.
Alifafanua kuwa, kila chama kizingatie ratiba na muda wa vibali wa kumaliza mikutano ya kampeni.
Alitumia
fursa hiyo pia kuwaomba wadau wa Ulinzi na Usalama kutoa ushirikiano
kama walivyofanya katika chaguzi zilizopita, kwa lengo la kudhibiti
vitendo vyenye kupelekea kuvuruga kampenzi na uchaguzi kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment