Wednesday, 26 February 2014

SIUNGI MKONO UTEUZI WA CHUJI,NA ERASTO TAIFA STARS



 
                      
Na Baraka Mbolembole
 Jana timu ya Soka ya Taifa ya Tanzania ilitajwa na shirikisho la
soka nchini, TFF. Shirikisho hilo lipo katika hatua za mwisho za
kuvunja mkataba na wa kocha Kim Poulsen ambao bado umebakiza miezi miwili, hivyo kutokana na kocha huyo kushindwa kuifikisha Tanzania katika michuano ya AFCON, katika mwaka 2013, kushindwa kuwa na matokeo mazuri  katika harakati za kufuzu kwa michuano ijayo ya kombe la dunia, kushindwa kuifikisha walau fainali za CECAFA, na matokeo mabaya
katika harakati zilizofeli za michuano ya CHAN iliyomalizika mwezi uliopita nchini Afrika ya kusini.
Ni sababu za muhimu ambazo TFF, wameona na wakati huu timu ikijiandaa na harakati za kufuzu kwa michuano ya AFCON 2015, nchini Morocco ni lazima wawe na kocha mwenye mkakati wa kuifikisha Tanzania katika fainali hizo ambazo mara ya mwisho, Taifa Stars ilishiriki mwaka 1980, nchini Nigeria.

Katika orodha hiyo wapo wachezaji waliostahili kuwemo ila wapo pia ambao hawakuwa na sifa za kuwemo kikosini kwa sasa. Stars itacheza na timu ya Taifa ya `Zimbabwe, mwanzoni mwa mwezi ujao katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki kwa mujibu wa kalenda ya FIFA, Shirikisho la soka Ulimwenguni.

 Sipingani na uamuzi wa kiungo Athumani Iddi ' Chuji', lakini je mchezaji huyo alikuwa na sifa za kuwepo Stars kwa wakati huu akiwa hajapata muda wa kutosha wa kucheza katika klabu yake
tangu tarehe 20, Disemba? Haya ni makosa ambayo wakati mwingine yanaleta ugumu wa timu kufanikiwa. 
Timu ya Taifa ni mkusanyiko bora wa wachezaji wa nchi husika katika wakati husika. Ndiyo, Chuji atakuwa akiwasaidia wachezaji vijana kupata uzoefu

Hivi, huyu kijana wa Academy ya Allience, Athanas  Mdamu, imekuwaje akaachwa wakati kuna wachezaji vijana kama Elius Maguli, Juma Luizio wanaocheza katika klabu zao na kufanya vizuri wasipewe nafasi. Ndiyo hata kama ni mchezaji mzuri, huko ni kuikosea heshima ligi kuu yetu.
Ni kuwakosea heshima wachezaji wengine. Nafikiri vijana kama hawa wanatakiwa kucheza katika timu za Taifa za vijana, na si moja kwa moja Stars. Hamis Mcha, Erasto Nyoni, ni maingizo ambayo yanathibitisha kuwa bado hakuna usawa wakati wa uteuzi wa wachezaji muhimu wa timu ya Taifa. Wateuaji wanaendeshwa kwa hisia za kukariri.

Michael Aidan, Hassan Mwasipili, Edward Charles ni wachezaji ambao wametoka nje ya Dar es Salaam, katika vilabu vya Ruvu Shooting, JKT Ruvu, na Mbeya City, ila kukosekana kwa wachezaji kama Himid Mao na Said Mourad, Luizio, Maguli, ni maamuzi mabaya na yanayoonesha kuwa timu imara ya Taifa ya Tanzania itakuwa ni ngumu kupatikana kwa kuwa uteuzi huu wa siku ya jana unaonesha wazi kuwa ndani ya TFF, kuna ukiritimba mkubwa. 
Uwepo wa Chuji,Erasto, Mdamu, ni sawa ila wapo wachezaji ambao wanasifa zaidi yao kwa sasa . Mara zote tumekuwa
tukikosoa kuhusu uteuzi mbaya wa timu ya Taifa na huu uliofanywa na watu wa mpira ni mbovu zaidi

0 comments: