Usiku
wa kuamkia February 26 uliingia kwenye headline kwenye mitandao ya
kijamii na hii ni baada ya kusambaa kwa video na picha zinazomuonyesha
Pancras Ndaki Charles au Pnc kupiga magoti mbele ya Ostaz Juma Namusoma
kama kumuomba msamaha wa kurudi kwenye kundi.
Picha hizo zimeibua mambo mengi sana na baadhi ya wasanii na wadau
wakubwa wakidai kuwa Ostaz Juma Namusoma kamdharirisha Pnc,miongoni mwa
wasanii walioonekana kukerwa zaidi na kitendo hicho ni pamoja na member
wa zamani wa kundi hilo Kitale na wadau wengine kama Adam Juma,Suma
Mnazaleth,Said Fela na wengine wengi.
Hii
ni nafasi naomba tuitumie kumsikiliza Pnc mwenyewe akielezea hali
hiyo>>’‘Kuomba samahani hiki kitu sijaona kama ni kitu kibaya
kwangu hata kupiga goti kumuomba samahani- kwa sababu hata baba yangu
siku zote nilipokuwa nikimkosea yaani ilikua kawaida yangu,baba bana
nisamehe yaani kwa kwa upande wetu ni heshima tu nimechukulia’
‘Kwa sababu mwenyewe anadai yeye hajazijichapisha yeye zile
picha,tulikuwa wengi kifupi sijajua siwezi kumlaumu nikasema ostaz
umechapisha inshu zangu, kikubwa kuhusu haya mambo mi napotezea
naangalia mambo yangu’
‘Unajua ostaz wanamchukulia kama kaka yangu wakinipigia simu ndugu
zangu wananilaumu wewe umemfanya nini ostaz,tumeshaongea na ostaz
kinachofuata sasa hivi ni kuingia studio na kufanya kazi zangu kama
kawaida’.
0 comments:
Post a Comment