WATOTO WAWILI WENYE UMRI WA MIAKA 6 WAFARIKI DUNIA WAKIWA WANAOGELEA KATIKA MADIMBWI YA MAJI.
WATOTO
WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA ANOLD ZAKAYO (06) MWANAFUNZI WA
DARASA LA KWANZA SHULE YA MSINGI MWANYANJE NA SELINA EMMANUEL (06)
MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI SHULE YA MSINGI MWANYANJE WALIFARIKI DUNIA
WAKIWA WANAOGELEA KWENYE MADIMBWI YA MAJI KATIKA MTAA WA NSALAGA. TUKIO
HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 22.02.2014 MAJIRA YA SAA 11:00HRS ASUBUHI
HUKO UYOLE KATA YA NSALAGA TARAFA YA IYUNGA JIJI NA MKOA WA MBEYA.
CHANZO CHA VIFO HIVYO NI BAADA YA MAREHEMU HAO KUZIDIWA NA MAJI AMBAYO
YAMETOKANA NA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA PINDI WANAOGELEA NA WATOTO
WENZAO. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI
ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWA MAKINI KWA KUWEKA
UANGALIZI WA KUTOSHA KWA WATOTO WAO ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA
KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUFUNIKA/KUFUKIA/KUZIBA
MITARO/VISIMA/MASHIMO YALIYO WAZI KWANI NI HATARI KWA WATOTO HASA KATIKA
KIPINDI HIKI CHA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA ILI KUEPUKA MADHARA
YANAYOWEZA JITOKEZA.
MCHUNGAJI WA KANISA LA TAG SONGWE MKOA WA MBEYA AKUTWA AMEFARIKI DUNIA SHAMBANI KWAKE.
MCHUNGAJI
WA KANISA LA TAG SONGWE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MARIA LEONARD (38)
MKAZI WA IGIDA AKUTWA AMEFARIKI DUNIA KWENYE SHAMBA LAKE LA MAHINDI.
TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 22.02.2014 MAJIRA YA SAA 12:30HRS
MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA IGIDA, KATA YA UTENGULE USONGWE, TARAFA YA
SONGWE WILAYA YA MBEYA VIJIJINI. AWALI MNAMO TAREHE 15.02.2014 MAREHEMU
ALIWAAGA WAUMINI NA MAJIRANI KUWA ANAKWENDA KUHUDHURIA MAZISHI KATIKA
KIJIJI CHA ISUNGO WILAYA YA MBOZI NA TOKEA HAPO MAREHEMU HAKUONEKANA
NYUMBANI MPAKA MAITI YAKE ILIPOONEKANA. MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA
UMESHAHARIBIKA HUKU PEMBENI KUKIWA NA JEMBE LAKE. TAARIFA ZA AWALI
ZINASEMA HUENDA MAREHEMU ALIPIGWA NA RADI WAKATI AKIWA SHAMBANI KWAKE.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI
ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA JAMII KUEPUKA KUKAA/KUJIFICHA KARIBU NA
MITI MIKUBWA WAKATI MVUA INANYESHA KWANI NI HATARI.
WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI 1. MAJUTO MWALYAZI
(34) MKAZI WA ISANGA NA 2. QUEEN NDAMBO (55) MKAZI WA SINDE WAKIWA NA
POMBE HARAMU YA MOSHI UJAZO WA LITA 57 1/4.
WATUHUMIWA WALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOENDESHWA NA JESHI LA POLISI
MNAMO TAREHE 22.02.2014 MAJIRA YA SAA 09:30HRS ASUBUHI ENEO NA KATA YA
SINDE, TARAFA YA SISIMBA JIJI NA MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA NI WAUZAJI NA
WATUMIAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI
ZINAENDELEA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA
POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUTUMIA
POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI
KWA AFYA YA MTUMIAJI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI.
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA YOHANA MGAYA (33) MFANYABIASHARA,
MKAZI WA ULAMILA AKIWA NA POMBE KALI AINA YA DOUBLE PUNCH VIROBA 17 NA
BULLET CHARGER VIROBA 09 ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI. MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 22.02.2014 MAJIRA YA SAA 21:00HRS USIKU HUKO
KATA YA IGURUSI, TARAFA YA ILONGO WILAYA YA MBARALI. MTUHUMIWA NI
MUUZAJI WA POMBE HIZO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI
ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA
KUUZA/KUSAMBAZA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA NA HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WAHAMIAJI HARAMU 07 RAIA WA NCHINI PAKISTAN.
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WAHAMIAJI HARAMU SABA [07] RAIA
WA NCHINI PAKISTAN WAKIWA NA MWENYEJI WAO ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA
HALFAN SARAI (37) MKAZI WA GONGO LA MBOTO JIJINI DAR-ES-SALAAM.
WAHAMIAJI HAO HARAMU WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 22.02.2014 MAJIRA YA SAA
21:00HRS USIKU HUKO KATIKA KATA YA IGURUSI TARAFA YA ILONGO WILAYA YA
MBARALI WAKIWA WANASAFIRISHWA KATIKA GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.396
CSU AINA YA TOYOTA NOAH KUELEKEA NCHI JIRANI YA ZAMBIA. TARATIBU ZA
KUWAKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZINAENDELEA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI
ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA KWA JESHI LA POLISI
NA MAMLAKA HUSIKA JUU YA WATU WANAOWATILIA MASHAKA HASA WAHAMIAJI
HARAMU ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATATU WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI.
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATATU 1. RASHID HAULO (32)
2. SALUM ADINANI (30) NA 3.SIMAUNGANA ATHUMANI (32) WOTE WAKAZI WA
MADEBENI WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 20.
WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 22.02.2014 MAJIRA YA SAA 22:00HRS
USIKU HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MADEBENI, KATA YA ITEWE, TARAFA YA
KIWANJA WILAYA YA CHUNYA. WATUHUMIWA NI WAUZAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU
ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA TABIA YA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA
SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Signed by:
[ROBERT MAYALA – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment