Saturday, 22 February 2014

MWALIMU AUAWA BAADA YA KUMCHINJA MWANAFUNZI

 
Mwalimu wa madrasa ya Ali Munawar, ustaadhi Mohamed Ngulanjwa (36) wa Mbagala Mianzini jijini Dar es Salaam, ameuawa baada ya kumchinja mwanafunzi wake.
Ustaadhi huyo aliyekuwa mwalimu wa madrasa na shule ya awali ya Ali Munawar, alimchinja mwanafunzi huyo jana saa 12.10 jioni kwenye eneo la madrasa baada ya kutenganisha kichwa na kiwiliwili
(hudugu)
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, Jonathan Shana, akizungumzia mauaji hayo , alisema tukio hilo la kinyama, lilishuhudiwa na wananchi waliomuua ustadhi huyo.
Alisema baada ya mwalimu kumuua mwanafunzi wake wa kiume alichukua kisu alichotumia pamoja na msahafu na kukimbia.
"Ilidaiwa kuwa alimchukua mtoto huyo , kumlaza chini kisha kumchinja kwa kutenganisha kichwa na kiwiliwili na kutelekeza vipande vya mwili wake kwenye varanda," alisema Kamanda Shana.
Baada ya mauaji hayo mtuhumiwa alianza kukimbia lakini wananchi walimvamia na kumshambulia kwa mawe na kila silaha iliyokuwa karibu na kumuua papo hapo.
Shana alieleza kuwa polisi walifika eneo la tukio na kuchukua maiti hizo na kuzipeleka hospitali ya Temeke.
Hata hivyo alisema jina la mtoto huyo mwenye umri kati ya miaka 10- 12 halikufahamika na polisi inaendelea na uchunguzi.
ASante kwa kutembelea blog yetu ya mbeyagreennews MUNGU AKUBALIKI (GOD BLESS)
CHANZO: NIPASHE

0 comments: