Mugabe ametawala Zimbabwe tangu mwaka 1980.
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amefikisha miaka 90 leo na kuwa rais mkongwe zaidi barani Afrika.
Amekuwa Rais wa Zimbabwe tangu nchi hiyo ijipatie uhuru mwaka 1980.
Hata
hivyo sherehe za siku ya kuzaliwa kwake zitafanyika Jumapili huku
kukiwa na tetesi kuhusu hali yake mbaya ya kiafya pamopja na mvutano
kuhusu uongozi wa chama tawala.
Sherehe hizo zinakisiwa kugharimu dola milioni moja.
Mugabe
alichukua mamlaka mwaka 1980 wakati Zimbabwe ilipojinyakulia uhuru
kutoka kwa Uingereza na amekuwa akisemekana kuwa mgonjwa sana.
Amekuwa akienda nchini Singapore, kwa ukaguzi wa kimatatibabu mara kadhaa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Taarifa zilifichuliwa mwaka 2008 kuwa Mugabe anaugua Saratani ya tezi kibofu, madai ambayo serikali ilikanusha vikali.
Taarifa hizi ziwe za kweli au za uongo, cha mno ni kwamba kwa sasa Zanu-PF kinajiandaa kwa maisha bila ya Rais Mugabe.
Hata
hivyo mnamo siku ya Alhamisi Mugabe alisema hakuna umuhimu wowote wa
kuanza kuzungumzia swala la Urithi wakati yeye yungalipo.
“kwa
nini swala hili lijadiliwe wakati muda bado? Je muda umewadia wa
kulizungumzia?” alinukuliwa akihoji na gazeti la The Herald nchini
Zimbabwe
“uongozi bado upo . Yaani bado nipo,” alisema Mugabe.
Chanzo: BBC swahili
ASante
kwa kutembelea blog yetu ya mbeyagreennews MUNGU
AKUBALIKI (GOD BLESS)
0 comments:
Post a Comment