>>MECHI: Jumatatu Februari 3 SAA 5 Usiku
>>UWANJA: Etihad
Usiku huu, Manchester City, ambao wako
Nafasi ya Pili Pointi 2 nyuma ya Arsenal, na Chelsea walio Nafasi ya 3,
Pointi 3 nyuma ya Man City, wanakutana kwenye Mechi ya Ligi Kuu England
ambayo matokeo yake yatafafanua zaidi nini kitajiri mbio za Ubingwa
Msimu huu.
Hii ni Mechi ya Pili kukutana Msimu huu na katika Mechi ya Kwanza huko Stamford Bridge, Chelsea waliibuka kidedea kwa Bao 2-1.
Lakini Man City, wakiwa kwao Etihad, ni
mnyama mkali ambae anasaka ushindi wake wa 12 mfululizo na Msimu
uliopita Uwanjani hapo Man City iliinyuka Chelsea Bao 2-0.
Kwenye Mechi hii, Timu zote zitawakosa
Mastraika wao hatari, Sergio Agüero na Fernando Torres, ambao waliziona
nyavu walipokutana Stamford Bridge mapema mwanzoni mwa Msimu huu.
Hali za Wachezaji:
Manchester City
-Majeruhi: García, Nasri, Agüero
-Mfungaji Bora: Agüero Bao 15
Chelsea
-Majeruhi: Torres, Van Ginkel
-Mfungaji Bora: Hazard Bao 9
Uso kwa Uso:
-Manchester City wameshinda Mechi 4
zilizopita dhidi ya Chelsea Uwanjani Etihad kuanzia Msimu wa 2008/09 na
mara ya mwisho Carlos Tevez na Yaya Toure walifunga waliposhinda 2-0.
-Msimu huu, Chelsea iliifunga Manchester
City Bao 2-1 Mwezi Oktoba kwenye Ligi kwa Bao za Andre Schurrle na
Fernando Torres na Bao la City kufungwa na Sergio Aguero.
-Mara ya mwisho kwa Chelsea kuipiga City dabo, yaani Mechi zote mbili za Ligi katika Msimu mmoja, ni Msimu wa 2008/09.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
AKIBA:
Manchester City: Pantilimon, Nastasic, Clichy, Richards, Jovetic, Lescott, Rodwell, Boyata, Milner
Chelsea: Schwarzer, Hilário, Kalas, Cole, Ake, David Luiz, Mikel, Salah, Willian, Ba, Schürrle
Refa: Mike Dean
0 comments:
Post a Comment