TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 24.05.2014.
- MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPIGWA JIWE KICHWANI.
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA KUKUTWA NA BHANGI.
TUKIO LA KWANZA.
MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPIGWA JIWE KICHWANI.
MTU MMOJA BARIKO MWAKASISILE
[40], MKAZI WA KIJIJI CHA NYELELE- BUJONDE WILAYA YA KYELA ALIFARIKI
DUNIA WAKATI ANAENDELEA KUPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA WILAYA
YA KYELA TAREHE 23.05.2014 MAJIRA YA SAA 16:00HRS ALASIRI.
MAREHEMU ALIPIGWA JIWE KICHWANI
NA LUPAKISYO JACOB, MKAZI WA KIJIJI HICHO. TUKIO HILO LILITOKEA TAREHE
19.05.2014 MAJIRA YA SAA 23:00HRS USIKU HUKO KATIKA KITONGOJI CHA
NYELELE, KIJIJI NA KATA YA BUJONDE TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA
KYELA. CHANZO CHA TUKIO HILO KINACHUNGUZWA NA MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA
BAADA YA TUKIO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPOKIMBILIA MTUHUMIWA AZITOE
KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
KATIKA MSAKO.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAWASHIKILIA WATU WAWILI [02] KUTOKANA NA MISAKO MBALIMBALI
ILIYOFANYIKA. KATIKA TUKIO LA KWANZA JESHI LA POLISI LINAMSHIKILIA
MTU MMOJA THOMAS BENEDICTO [30], MKAZI WA MBUGANI – KYELA KWA KUKUTWA
NA BHANGI KETE 62 ZENYE UZITO WA GRAMU 460 PAMOJA NA BHANGI AMBAYO BADO
HAIJASOKOTWA GRAM 500,YOTE IKIWA NA UZITO WA GRAM 960.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE
23.05.2014 MAJIRA YA SAA 08:30HRS ASUBUHI HUKO ENEO LA KALUMBULU, KATA
YA KYELA – KATI, TARAFA YA UNYAKYUSA. MTUHUMIWA NI MTUMIAJI NA MUUZAJI
WA BHANGI, TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.
KATIKA TUKIO LA PILI JESHI LA
POLISI LIMEMKAMATA MTU MMOJA MWANGOTA MWANGOTA [40], MKAZI WA KIJIJI
CHA IBUNGU KYELA KWA KUKUTWA NA BHANGI KETE 70 ZENYE UZITO WA GRAMU
350.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE
23.05.2014 MAJIRA YA SAA 09:45HRS ASUBUHI HUKO ENEO LA MBUGANI, KATA
YA KYELA KATI, TARAFA YA UNYAKYUSA. MTUHUMIWA NI MTUMIAJI NA MUUZAJI
WA BHANGI NA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Imesainiwa na
[ B.N.MASAKI – ACP ].
Kny: KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment