Kaimu
Mkurugenzi wa Biashara wa Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL) Bw.
Juma Boma (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii
Mhe.Lazaro Nyalandu wakati wa uzinduzi wa safari ya ATCL ya Dar es
Salaam -Arusha – Zanzibar, wakitumia ndege yao yenye uwezo wa kuwabeba
abiria 50 aina ya Bombardier Dash-8. Uzinduri ulifanyika Jumatano jioni.
(Picha na mpiga picha wetu)
Kaimu
Mkurugenzi wa Biashara wa Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL) Bw.
Juma Boma (wa kwanza kulia) akishuka kutoka katika ndege ya shirika hilo
aina ya Bombardier Dash-8 akifuatwa na Waziri wa Maliasili na Utalii
Mhe.Lazaro Nyalandu (wapili kulia) wakati wa uzinduzi wa safari za ndege
hiyo kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar ikipitia Arusha. Hafla hiyo
ilifanyika Jumatano jioni. (Picha na mpiga picha wetu)
Kapteni
Richard Shaidi (kulia) akizungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii
Mhe.Lazaro Nyalandu (kushoto) mara tu baada ya ndege ya Air Tanzania
(ATCL) kutua katiwakati uwanja wa ndege wa Arusha ikiwa ni uzinduzi wa
safari yake ya kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar ikipitia Arusha.
Shirika hilo la ndege limepanga kusafiri mara sita kwa wiki ikitumia
ndege yake ya aina ya Bombardier Dash-8. (Picha na mpiga picha wetu).
Kaimu
Mkurugenzi wa Biashara wa Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL) Bw.
Juma Boma (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
wakati wa uzinduzi wa safari ya ATCL ya Dar es Salaam- Arusha –
Zanzibar, wakisafiri mara sita kwa wiki kwa kutumia ndege yao ya aina ya
Bombardier Dash-8. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Bw. John
Mongela. (Picha na mpiga picha wetu).
Mkuu
wa Wilaya ya Arusha Mjini Bw. John Mongela (kushoto) akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) maara baada ya kupokea wageni na
abiria waliosafiri na ndege ya Air Tanzania, Jumatano jioni wakati wa
uzinduzi wa safari ya ATCL ya Dar es Salaam -Arusha– Zanzibar, wakitumia
ndege yao ya aina ya Bombardier Dash-8. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa
Biashara wa Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL) Bw. Juma Boma.
(Picha na mpiga picha wetu).
Kaimu
Mkurugenzi wa Biashara wa Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL) Bw.
Juma Boma (kulia) akibadilisha kadi ya mawasiliano na Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais (Utawala Bora)-wa Zanzibar- Dk. Mwinyihaji Haji Makame
(kushoto) aliyekuwa miongoni mwa abiria waliopanda ndege hiyo Jumatano
jioni wakati wa uzinduzi wa safari ya ATCL ya Dar es Salaam- Arusha–
Zanzibar ikitumia ndege yake ya aina ya Bombardier Dash-8. (Picha na
mpiga picha wetu).
Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA
la Ndege la Taifa, Air Tanzania (ATCL) limerejea katika anga za Arusha
na Zanzibar na kuahidi kusafiri katika maeneo hayo yenye vivutio bora
vya kiutalii mara sita kwa wiki.
Katika
safari hiyo ya uzinduzi ya kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar kupitia
Arusha, kulikuwa na mawaziri wawili wa pande zote za muungano ambao
walionyesha kufurahishwa na safari hiyo, mbali na kutoa nasaha kwa
shirika hilo.
Ikitokea
Dar es Salaam kwenda Arusha, alikuwemo Waziri wa Maliasili na Utalii
Bw. Lazaro Nyalandu na wakati wa kutoka Zanzibar kwenda Dar es Salaam,
alipanda Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Zanzibar (Utawala Bora),
Dkt. Mwinyihaji Haji Makame, wote wakiashiria kuwa safari hiyo
imerejesha matumaini ya kuwaunganisha watalii kutoka Arusha kwenda
Zanzibar na kurudi Dar es Salaam.
Akizungumza
mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Arusha, Mh. Nyalandu,
alisema kurejea kwa ndege ya shirika hilo la Taifa katika njia ya Arusha
na Zanzibar kutakuza sekta ya utalii na kurahisisha uunganishwaji wa
maeneo hayo muhimu yenye vivutio vikubwa vya utalii.
“Ninayofuraha
ya kuwataarifu watalii, wageni wanaotembelea nchi yetu na watanzania
wenzangu kuwa Air Tanzania sasa imerudi angani. Nimekuwa miongoni mwa
abiria wa kwanza kusafiri na ndege hii kuja hapa Arusha, kwa hiyo nataka
kuwahakikishia wote kuwa usafiri wa Air Tanzania ni tulivu, wanatoa
huduma nzuri ndani ya ndege, ni salama na utafurahia safari yako.
“Uzinduri
wa safari hii unadhihirisha kwamba sasa ushindani wa kweli katika sekta
ya usafiri wa anga umeanza. Shirika la Air Tanzania linatakiwa
kuhakikisha linaendeleza dhamira yake ya kutoa huduma bora ili liweze
kurejesha imani lililokuwanayo kwa abiria wake walio wengi,” alisema
Nyalandu.
Naye,
Kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa ATCL Bw. Juma Boma alisema safari ya
Dar es Salaam – Arusha – Zanzibar ni sehemu ya mkakati wa shirika lake
wa kutanua huduma zake katika maeneo mengi iwezekanavyo.
“Tunajivunia
kuendelea kutekeleza dhamira yetu ya kuimarisha huduma zetu tukiwa kama
shirika la Ndege la Taifa. Tukilenga kuendelea kutanua wigo wa huduma
zetu ndani ya nchi na kimataifa.
“Lengo
letu kubwa kama Shirika la Ndege la Taifa ni kuendelea kutoa huduma
zenye gharama nafuu, vile vile kuongeza uwezo wa abiria kusafiri kwa
wakati wao”. Ndiyo sababu tumeondoa adhabu kwa wale abiria wanaochelewa
kufika uwanja wa ndege au kushi ndwa kufika kabisa siku ya safari na
wanaobadilisha tarehe za safari zao,” alisema.
Aidha,
Waziri wa Zanzibar, Mwinyihaji Haji Makame, alisema inatia moyo kuona
ATCL ikirejesha safari zake Zanzibar baada ya kusitisha huduma zake
katika kisiwa hicho kwa zaidi ya miaka minne, lakini aliwataka ATCL
kufuata muda na kuhakikisha wanapunguza adha ya usitishaji wa safari
endapo wanataka kurejesha imani miongoni mwa abiria walio wengi.
Akizungumza
baada ya kupokea safari hiyo ya uzinduzi katika uwanja wa ndege wa
Arusha, Mkuu wa Wilaya ya Arusha mjini, Bw. John Mongela alisema uanzaji
wa safari hizo za ATCL katika Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki na Geneva ya Afrika umerejesha sifa iliyokuwa nayo ndege hiyo
ya taifa kipindi cha nyuma wakati wa mikutano ya kimataifa jijini
Arusha.
“Hii
ni hatua ya busara sana kwa ATCL. Jiji la Arusha alitoi tu fursa ya
ndege hii kusafirisha watalii moja kwa moja kutoka Dar es Salaam kuja
Arusha na kuwaunganisha kwenda Zanzibar, bali pia inawapa fursa ya
kusafirisha viongozi wa kimataifa wanaosafiri mara kwa mara kuja Arusha
kwa ajili ya mikutano,” alisema.
Kwa sasa, ATCL itakuwa ikitumia ndege yake aina ya Bombardier Dash – 8 yenye uwezo wa kubeba abiria 50 katika njia hiyo.
0 comments:
Post a Comment