Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisikiliza maelezo kutoka mkwa Dr. Daniel Mbwambo Meneja wa Maabara katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Manyara wakati alipotembelea hospitali hiyo na kukagua utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kusikiliza kero za wananchi ikiwa ni pamoja na kuzitafutia ufumbuzi, Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi, Akizungumza hospitalini hapo Katibu Tawala wa mkoa wa Manyara Injinia Omar Chambo amesema ziara ya Katibu Mkuu Kinana kwenye hospitali ya Kilutheri ya Hydom wilayani Mbulu imezaa matunda. baada ya wizara ya Afya na Ustawi jaimii kumtaarifu kwamba anatakiwa kuwaajiri watumishi 93 wa hospitali hiyo ambao walikuwa wanahamia serikalini katika hospitali mbalimbali hivyo wanaingia katika utaratibu wa ajira ya serikali na wanatakiwa kubaki hospitalini hapo kwa utumishi wao, Lakini pia serikali katika utaratibu wake wa ruzuku imeiongezea ruzuku hospitali hiyo inayofadhiliwa na nchi Sweden kwa miaka 50 kutoka shilingi milioni 200 mpaka shilingi milioni 320 kwa mwaka ili kuboresha zaidi huduma za hospitali hiyo ambayo imekuwa ikihudumia zaidi ya mikoa sita ya kaskazini na kanda ya kati. Katika picha kushoto ni Katibu tawala wa mkoa wa Manyara injinia Omary Chambo MANYARA)
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na mganga mkuu wa mkoa wa Manyara Dr. Ally Uredi kulia wakati akikagua mradi wa ujenzi wa hospitali hiyo, Kushoto ni Mbunge wa jimbo la Babati Mjini Mh. Kisyeri Chambili.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na mganga mkuu wa mkoa wa Manyara Dr. Ally Uredi kushoto, yanayoonekana nyuma ni majengo ya hospitali hiyo.
Baadhi ya watumishi wa hospitali hiyo wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na watumishi wa hospitali hiyo mara baada ya kukagua majengo mbalimbali hospitalini hapo kutoka kushoto ni injinia Omary Chambo katibu tawala wa mkoa huo, Mh. Dr. Mary Nagu Mbunge wa jimbo la Hanang na Waziri wa Uwezeshaji, Mh. Kisyeri Chambiri mbunge wa jimbo la Babati mjini na Mganga mkuu wa mkoa wa Manyara Dr. Ally Uredi.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisikiliza taarifa ya ujenzi wa zahanati ya kata ya Nakwa.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua mradi wa kisima cha maji safi katika kata ya Nakwa, kutoka kushoto ni Khalid Mandia Muu wa wilaya ya Babati,Erasto Mbwilo Mkuu wa mkoa wa Manyara na Dr. Mary Nagu Waziri wa Uwezeshaji na mbunge wa jimbo la Hanang
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza jambo na watoto hawa ambao majina yao hayakufahamika mara moja huku akiwaonyesha saa yake ya mkononi.
Baadhi ya majengo ya Hospitali ya rufaa ya Manyara yanavyoonekana.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiaini kitabu mara baada ya kuwasili hospitalini hapo kushoto niJulieth Dias Muuguzi Mfawidhi hospitali ya mkoa wa Manyara. Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wafanyakazi mbalimbali wa hospitali hiyo walipokuwa wakimpokea.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Julieth Dias Muuguzi Mfawidhi Hospitali ya mkoa wa Manyara wakati alipowasili hospitalini hapo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akielekea kukagua nyumba ya mwalimu katika shule ya sekondari ya Komoto.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua madarasa ya shule ya sekondari ya Komoto wilayani Babati.
0 comments:
Post a Comment