Na Baraka Mpenja Dar es salaam
WASHAMBULIAJI wa kimataifa wa
Tanzania, Mbwana Ally Samata na Thomas Emmanuel Ulimwengu kesho jumapili
wanatarajia kuiongoza TP Mazembe katika mchezo wa hatua ya makundi ya
ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya wapinzani wao wakubwa, AS Vita
mjini Lubumbashi.
Timu hizi hasimu zitakutana katika
mchezo wa kesho zikiwa na kumbukumbu ya kusababisha maafa ya vifo vya
watu zaidi ya 15 katika mchezo wao wa ligi kuu ya DR Congo wiki za
karibuni.
Tukio hilo baya lilitokea mjini
Kinshasa baada ya mashabiki wa AS Vita kutoridhishwa na kipigo cha bao
1-0 kutoka kwa wapinzania wao TP Mazembe.
Mchezo wa kesho umevuta hisia za
mashabiki wengi wa soka, kwani timu hizi zinapokutana, upinzani
unakuwabmkubwa mno nje ya uwanja na ndani ya uwanja.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment