HOSPITALI
ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru, inakabiliwa na upungufu wa shuka 300 na
blanketi 200, kutokana na ongezeko kubwa la wagonjwa kila
siku.
Akizungumzia upungufu huo jana hospitalini hapo, wakati
akipokea msaada wa shuka nyeupe 100 na blanketi 30 toka kwa Kanisa la
Calvary
Temple la Kilombero Jijini Arusha,ambalo linaadhimisha miaka 75
tangu lianzishwe, Mganga Mfawidi wa Hospitali hiyo, Dk. Josiah Mlay,
alisema
upungufu ni mkubwa wa vitu hivyo ukizingatia wanakwenda kipindi cha baridi kali.
Alisema kuwa shuka na blanketi
walizonazo kwa sasa nyingi zimechakaa kutokana na kemikali wanazotumia
kufulia wakati zinapochafuka wodini,
hivyo wanahitaji shuka na blanketi zingine haraka kabla ya msimu wa baridi haujaanza.
“Kwa nyie kutuletea hivi vitu
tunashukuru sana na mtabarikiwa, kwani bado tuna upungufu wa itu hivi
mkubwa na tunaomba wadau wengine
wajitokeze kutusaidia kabla ya msimu wa baridi haujaanza,”alisema.
Dk. Mlay alisema kwa sasa
hospitali hiyo inachangamoto kubwa ya ongezeko la wagonjwa na huku
mahitaji yao yakipungua, kutokana na
wingi wao, hivyo wanahitaji wasamaria wema wajitokeze
kuwasaidia. Mahitaji mengine wanayohitaji hospitalini hapo alitaja kuwa
pamoja na
vifaa vya maabara navyo ni vichache,hivyo wanaomba msaada
kwa wasamaria wema na sio kuiachia serikali ambayo inamajukumu
mengi. Kwa upande wake Emmanuel Mbwiga ambaye ni Mzee wa Kanisa la
Calvary
Temple la Kilombero Jijini Arusha,
akitoa msaada huo alisema mbali na msaada huo pia kupitia vituo vyao
mbalimbali wametoa msaada kwenye
vituo vya yatima vya Huruma Kwamurombo,Monduli,Esso.
Pia misaada mingine imetolewa
shule za msingi Mwangaza, Olsinyai Sombetini na Ngarenaro, lengo kubwa
kusaidia watu wenye shida ili
wapate faraja nao katika kuadhimisha kilele cha kanisa hilo kitakachofanyika Kitaifa Mbeya Julai mwaka huu.
Mbwiga alisema vitu walivyotoa
maeneo hayo ni Sabuni, ndoo za mafuta, mchele, nguo,
mahindi,daftari,soksi na vitu vingine vingi, ambavyo
vyote vina jumla ya shilingi milioni 3.
Hata hivyo alitoa wito kwa watu
wenye mapenzi mema kujitokeza kusaidia hospitali hiyo na maeneo yenye
uhitaji kama vitruo vya yatima
na shuleni, ili wabarikiwe zaidi.
0 comments:
Post a Comment