Monday, 26 May 2014

SERIKALI YAPOTEZA DOLA 581 KILA MWAKA

 

Dar es Salaam. Serikali imedaiwa kupoteza Dola za Kimarekani 581 milioni kila mwaka kutokana na ununuzi wa dawa za virutubisho vya madini kwa watoto chini ya miaka mitano na wanawake nchini.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji kutoka Taasisi ya Lishe Tanzania (TFNC), Benedict Jeje aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa mkutano wa wadau wa lishe uliokuwa ukijadili umuhimu wa viazi lishe kwa mtoto (viazi vya rangi ya chungwa au viazi karoti).
Dawa na virutubisho vinavyonunuliwa na Serikali ni pamoja na chanjo ya Vitamini 'A, Zink, chuma na folic. 
(Martha Magessa)

0 comments: