, WASEMA WAO SI CHAMA CHA SIASA
Waombolezaji wakitoa heshima zao huku wengine wakichukua picha za kumbukumbu |
Mhubiri aliyejitolea baada ya kanisa la Rc kususa kuendesha misa |
Marehemu enzi za uhai wake |
Kijana wa boda boda akifurahia kuwapokonya chepe wenzake |
Vijana wakizichapa ngumi kugombea kuzika |
Mwenyeji walikuwa watazamaji baada ya boda boda kuchukua jukumu zima la kuzika katikati ni mwenyekiti wa waganga wa tiba asilia mkoa wa Iringa Galusi Msekwa |
……………………………………..
Na www.mwandishiwetu.blogspot.com
MATUMAINI
ya vijana dhidi ya chama demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wilaya ya
Iringa mjini imeanza kutoweka baada ya jana dereva boda boda zaidi ya
200 kuwazuia viongozi wa Chadema kupeperusha wala kufunika bendera
za chama hicho katika bajaji iliyobeba mwili wa dereva mwenzao Abisai
Mdesa .
Vuta nikuvute hiyo ilitokea majira ya saa 4 asubuhi baada ya makada
wa Chadema kufika Chumba cha maiti katika Hospitali ya rufaa ya mkoa
wa Iringa wakiwa na bendera za Chadema kwa ajili ya kuwapa madereva
wa boda boda pamoja na kufunga katika bajaji iliyopaswa kubeba mwili
wa marehemu huyo bado bado msimamo wa boda bado ulionekana kupingana na
matakwa ya viongozi hao.
Vijana
hao walionesha kupinga msimamo wa makada hao wa Chadema kutoka
kufunika bendera wa chama chao katika jeneza la marehemu huyo wala
kupeperusha bendera ya chama chao katika msafara wa mazishi kwa madai
kuwa chama hicho cha boda boda Iringa si chama cha kisiasa na wala
hakina ubia na Chadema .
Wakizungumza
kwa jazba vijana hao waendesha boda boda boda walisema kuwa
wamesikitishwa na kitendo cha Chadema kutaka kujipatia umaarufu kupitia
mazishi ya dereva mwenzao huyu hali wakitambua kuwa wao si sehemu
ya Chadema.
Walisema
walikuwa tayari kuwashambulia kwa kipigo makada hao wanne wa Chadema
waliofika na bendera hizo iwapo wangeshindwa kuwasikiliza na
kuendelea na msimamo wao wa kufunga bendera.
Mwenyekiti wa chama cha boda boda na Bajaji mjini Iringa Joseph Mwambope aliwaeleza
waandishi wa habari kuwa hatua ya Chadema kutaka kujimilikisha
msiba huo ni kosa kubwa na kuwa wanachotambua kuwa marehemu hakuwa
kiongozi wa Chadema ila alikuwa ni mwanachama wa chama cha boda boda
hivyo mbali ya ndugu mwenye nafasi ya kuendesha mazishi hayo ni chama
cha boda boda na Bajaji pamoja na wasanii wenzake wa Mundu Sanaa Group
na sio chama chochote cha siasa.
“Tunaomba
ieleweke kuwa chama cha boda boda si chama cha kisiasa hivyo
haturuhusu Chadema ama CCM kuja na bendera za vyama vyao katika msiba
huu japo hatuwakatazi kuja na magari yao yakiwa na bendera za vyama
vyao ila sio kuleta bendera tufungi kwenye boda boda na bajaji zetu
“alisema Mwambope
Kuwa
imekuwa ni kawaida ya Chadema na vyama vingine kujipendekeza katika
misiba ambayo wanahisi ina waombolezaji wengi ili kutumia nafasi hiyo
kujitangaza kisiasa ila wakati wa kuuguza vyama hivyo huwa havitokei
kuuguza.
”
Huyu mwenzetu mbali ya kupata ajali ya pikipiki kwa siku zaidi ya nne
sasa alikuwa amelezwa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa na madereva
tulianza kuchangishana ili kumfanyia rufaa kwenda Hospitali ya Taifa
Muhimbili …..sasa kama Chadema ambao leo wanakuja na bendera wapo
kwanini wasingetoa usafiri wa kwenda Muhimbili kama si kutaka kuonekana
sasa baada ya kifo”
Katika
hatua nyingine vijana hao wa boda boda walilazimika kuzomea kada wa
Chadema aliyepewa kuweka shada kaburini kutokana na kushindwa
kukabidhi ahadi yao ya mchango wa shilingi 25000 ambazo waliahidi kwenye
daftari la waombolezaji bila kutoa pesa hiyo .
Kijana
huyo enzi za uhai wake alikuwa ni mpenzi wa Chadema ambae mara
kadhaa alionekana kupanda juu ya miti mirefu na kufunga bendera za
Chadema .
0 comments:
Post a Comment