Sunday, 25 May 2014

MOHAMED DEWJI ATOA MSAADA WA ZAIDI YA TSH. MILIONI 127 KWENYE TASISI ZA DINI ZAIDI 80 JIMBONI KWAKE

 
DSC_0025
Mbunge wa Singida Mjini, Mh. Mohammed Dewji (MO), akizungumza na viongozi wa Mahakama ya Qadhi wakati alipotembelea Mahakama hiyo kuona namna inavyohudumia waumini wa Dini ya Kiislamu katika kutatua migogoro ya ndoa.
DSC_0029
Sheikh wa Mahakama ya Qadhi, Ramadhani Kaoja akimweleza Mheshimiwa Mbunge shughuli za Mahakama hiyo pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili, Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Singida Mjini , Hamis Nguli, wa pili kulia ni Katibu wa Mahakama ya Qadhi, Alhajj B. Mlau.
DSC_0133
Mbunge wa jimbo la Singida Mjini MO akisalimiana na waumini wa Msikiti wa Kata ya Mtipa wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa Msikiti huo, ambapo mara baada ya kuona hatua zilizofikia za ujenzi huo aliahidi kutoa  Mabati 50 pamoja na mifuko 50 ya Saraji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo.
DSC_0171
MO akitoka kukagua ujenzi wa Msikiti wa kijiji cha Mangwanjuki kata ya Mtipa.
DSC_0237
Waumini wa Msikiti wa kijiji ch Mangwanjuki wakimsikiliza Mbunge wao Mheshimiwa MO.
DSC_0262
Baadhi ya wapiga kura wa kijiji cha Mangwanjuki wakipeana mikono ya Kheri na Mbunge wao.
DSC_0287

Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu wa Msikiti wa Mwankonko darajani wakimsikiliza Mbunge wao (hayupo pichani) wakati alipoendelea na zoezi la kutembelea nyumba za kuabudu zilizopo jimboni kwake.
DSC_0314
Jengo la wa Mwankonko darajani likiwa kwenye hatua Lenta, ambapo baada ya Mbunge kuona hatua hiyo ya nguvu za wananchi aliahidi Bati 50 na Mifuko ya Saruji 50.
DSC_0713
Mheshimiwa Mohammed  Dewji na baaadhi ya viongozi wa Msikiti wa kijiji cha Kisasida.
DSC_0729
Mbunge MO akizungumza na waumini wa Msikiti wa Kisasida, ambapo ameahidi kutoa msaada wa Mabati 100 na Mbao 100 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa Msikiti huo.
DSC_0738
MNEC wa Manispaa ya Singida, Hassan Mazala akitoa hamasa kwa wakazi wa Kisasida kushiriki Mkutano wa hadhara  ambao umeitishwa kwa ajili ya Katibu Mkuu CCM Taifa, Abdulrahman Kinana wa kuongea na wakazi wa jimbo la Singida Mjini utakaofanyika viwanja vya People’s Club.
DSC_0750
Mheshimiwa Mohammed Dewji akielekea kukagua ujenzi wa Msikiti wa Minga mjini Singida.
DSC_0336
Watoto wa Madrasa ya Msikiti wa Mwankoko Darajani wakimpokea Mbunge wao kwa mabango yenye ujumbe mbalimbali wakati alipotembelea ujenzi wa Msikiti huo.
DSC_0343
Mheshimiwa Mohammed Dewji akifurahia jumbe zilizoandikwa  na watoto wa Madrasa ya Mskiti wa Mwankoko Darajani.
DSC_0366
Baadhi ya watoto wa Mwankoko Darajani pamoja na wazazi wao wakifurahia ujio wa Mbunge wao.
DSC_0409
MO akizungumza na wananchi wa Mwankoko muda mfupi baada ya kukagua ujenzi wa Msikiti.
DSC_0434
Mchungaji wa Kanisa la FPCT kijiji cha Mtamaa akimpokea Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mh. Mohammed Dewji mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Kanisa hilo.
DSC_0464
Waumini wa Kanisa la FPCT Mtamaa wakitumbuiza wakati wa ziara Mbunge MO.
DSC_0467
Mbunge MO akijumuika na waumini wa Kanisa la FPCT kutoa burudani wakati wa ziara ya MO.
DSC_0503
Mheshimiwa MO akipokea zawadi ya Beberu la Mbuzi kutoka kwa waumini wa Kanisa la FPCT Mtamaa.
DSC_0505
MO akipokea zawadi ya Jogoo lililotolewa na waumini wa Kanisa la FPCT liwe linamuamsha asubuhi kwa ajili ya kwenda kazini.
DSC_0528
Mmoja wa wazee maarufu ambaye jina lake halikupatikana mara moja akifuatilia kwa makini hotuba ya Mbunge wake MO.
DSC_0542
Bango lililowekwa kwenye Msikiti wa Mtamaa.
DSC_0557
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Mtamaa wakifuatilia hotuba iliyokuwa inatolewa na MO baada ya kukagua ujenzi wa Msikiti wa Mtamaa.
DSC_0575
Mheshimiwa MO akizungumza na waumini wa Msikiti wa kijiji cha Mtamaa.
DSC_0630
Mheshimiwa MO akifurahia watoto wa kijiji cha Ng’aida kata ya Unyamiku wakati wa ziara yake.
DSC_0651
Mbunge MO akishiriki dua kwenye kijiji cha Msikiti wa Ng’aida.
DSC_0659
Mheshimiwa MO akiwa na watoto wa kijiji cha Ng’aida.
DSC_0670
Mheshimiwa MO akipokea zawadi ya Mbuzi kutoka kwa waumini wa Msikiti wa kijiji cha Ng’aida.


0 comments: