Saturday, 24 May 2014

MBEYA CITY YAANZA LEO MICHUANO MIPYA CECAFA BAADA YA JANA MABAO SABA KUFUNGWA KATIKA MECHI ZA UFUNGUZI


MABAO saba yametinga nyavuni katika mechi za ufunguzi za michuano ya mipya ya klabu ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) iitwayo Nile Basin jana nchini Sudan. Victoria University ya Uganda imeilaza 1-0 Malakia ya Sudan Kusini, wenyehi Al-Merreikh wameichapa 3-0 Polisi ya Zanzibar na wenyeji wengine, Al-Shandi wameilaza 2-1 Dkhill ya Djibouti.
Mbeya City wanaanza kazi leo Sudan
Wawakilishi wa Tanzania Bara, Mbeya watacheza mechi yao ya kwanza leo na Academie Tchite ya Burundi Saab 11:30 jioni kabla ya AFC Leopards ya Kenya kumenyana na Enticelles ya Rwanda Saa 2:00 usiku katika mchezo wa Kundi B. Michuano hiyo inashirikisha mabingwa wa Kombe la FA na washindi wa pili wa Ligi Kuu wa nchi wanachama wa CECAFA. Mbeya City imechukua nafasi ya Azam FC, washindi wa pili wa Ligi Kuu msimu uliopita, ambao wamejitoa. Simba SC ambao wangechukua nafasi ya Azam, wakati taarifa inakuja ya kufanyika kwa mara ya kwanza michuano hiyo, walikuwa wamekwishavunja kambi na wachezaji wao wote walikuwa wameruhusiwa likizo. 
Na Rodgers Mulindwa, KHARTOUM

0 comments: