Saturday, 24 May 2014

WAASI WA NCHINI MALI WASITISHA VITA

 
131214103536 mali security 304x171 ap 6f8f8
Na Hudugu Ng'amilo
Waasi nchini Mali wamekubali kusitisha vita siku mbili baada ya kuvishinda vikosi vya serikali katika mji wa kazkazini wa kidal.
Wanadiplomasia wamesema kuwa waasi hao wa kundi la Tuareg wanaotaka kujitenga waliahidi kusitisha vita baada ya kufanya mazungumzo na mwenyekiti wa umoja wa bara afrika Mohammed Abdel Azizi mjini Kidal.
Takriban wanajeshi 20 wa Mali waliuawa baada ya jaribio la kutaka kuuteka mji huo kutoka kwa waasi hao kufeli siku ya jumatano.
Waasi hao wameiambia BBC kwamba wanadhibiti eneo lote la kazkazini mashariki mwa Mali na sasa wanaelekea katika mji wa Gao.
Serikali imewashtumu waasi hao kwa kuungwa mkono na wapiganaji wa kundi la Al Qaeda.
CHANZO BBC

0 comments: