Mwili wa marehemu Geofrey Mlelwa (26) ukiwa katika gari la polisi katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa leo |
Baba mzazi wa kijana Mlelwa mzee Guriano Mlelwa kulia mwenye kofia akitazama gari hilo la polisi lenye mwili wa kijana wake |
Baba mzazi wa kijana Mlelwa mzee Guriano Mlelwa kulia mwenye kofia akitazama gari hilo la polisi lenye mwili wa kijana wake |
Gari la polisi likiwa na mwili wa kijana huyo |
MBALI ya jitihada mbali mbali
zinazofanywa na makampuni ya kutengeneza pombe kutoa tahadhari katika
chupa za pombe hizo kuwa unywaji pombe kupita kiasi ni hatari kwa
afya yako ila bado baadhi ya watu wameendelea kupuuza tahadhari hizo na
kuendeleza tabia ya kunywa pombe kupita kupindukia kiasi cha
kusababisha kuhatarisha maisha kama kijana mkazi wa Ipogolo mjini
Iringa Geofrey Mlelwa (26) aliyeamua kukatisha maisha yake kwa unywaji
pombe.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea
usiku wa kuamkia leo jumatatu katika eneo la Ipogolo mjini hapa ambapo
kijana huyo kuli katika soko kuu wa Manispaa ya Iringa akiwa na
wenzake alipoamua kuuchapa ulabu kiasi cha kushindwa kujitambua na
kupelekea kifo chake.
Wakizungunza na mwandishi wa habari
hizi baadhi ya mashuhuda walisema kuwa kijana huyo enzi za uhai wake
alikuwa ni mtu wa kunywa pombe za kienyeji aina ya ulanzi na bangi ila
siku hiyo ya tukio alionekana ni mwenye pesa hivyo kuachana na kunywa
pombe aliyoizoea na kuanza kunywa pombe ya kisasa kwa kuchanganya
Grant na viroba na ulanzi ndani ya chupa mmoja.
Hata hivyo walisema sanjari na
kumshauri kutumia pombe ambayo aliizoea ila bado aliendelea kupuuza na
kutumia pombe hiyo mpya kwake kwa kunywa kupita kiasi.
Mbali ya kunywa pombe hiyo ila
kijana huyo hakuweza kula chakula chochote toka alipoanza kunywa pombe
hiyo na alipozidiwa rafiki yake alimkokota na kumpeleka chumbani
kwao (getho) kabla ya asubuhi kuamka na kumkuta amekufa .
Baba mzazi wa kijana huyo mzee
Guriano Mlelwa allithibitisha kutokea kwa kifo cha kijana wake na
kuwa chanzo cha kifo hicho ni unywaji wa pombe kupita kiasi .
Alisema kuwa kwa kawaida kijana
wake anamtambua kama ni mlevi wa pombe na mtumiaji wa madawa ya kulevya
na kuwa hata katika chumba chake walimkutana na chupa ya pombe aina
ya grant ambayo ndani yake ilikuwa imechanganywa pombe mbali mbali
pamoja na viroba (konyagi).
Hivyo alisema anaamini kuwa
mchanganyiko huo wa pombe na matumizi ya dawa za kulevya ndio
umesababisha kifo hicho hivyo kuwashauri vijana kuachana na matumizi
ya pombe kupita kiasi na madawa ya kulevya kwani wakiendelea
kilichomuua mwenzao ndicho kitakachowaua pia.
0 comments:
Post a Comment