Katibu
Mkuu Dkt.Servacius Likwelile akiwa na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo
ya Afrika (AfDB) Kanda ya Afrika Mashariki Nd. Gabriel Negatu katika
Mkutano uliofanyika katika ukumb wa Ecobank Jijini Kigali Rwanda.
Mh.Waziri
wa Fedha Saada Mkuya Salum akijadiliana jambo na mmoja wa washiriki wa
Mkutano wa 49 wa Benki ya Maendeleo ya Afrika unafanyika Kigali Rwanda.
Pembeni ni mwa Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt.Servacius
Likwelile na msaidizi wa Waziri Bw.Thomas Mabeba.
Waziri
wa Fedha Mh.Saada Mkuya Salum akiwa na baadhi ya wajumbe wa mkuatno
mkuu wa mwaka wa benki ya maendeleo ya Afrika uliofanyika Kigali Nchini
Rwanda.
……………………………………………………………………
Mkutano
Mkuu wa 49 wa Benki ya Maendeleo ya Afrika umemalizika Jijini
Kigali,Rwanda kwa Viongozi wa Benki kuahidi kujenga Afrika ambayo ni
itakuwa na Umoja,mshikamano na yenye miundombinu ya uhakika.
Rais
wa Benki ya Maendeleo ya Afrika,Dkt. Donald Kaberuka amesema Benki
itasaidia utekelezaji wa mipango bora ambayo itatokana na majadiliano
yatakayofikiwa kwenye vikao nchi wananchama. Miongoni mwa vipaumbele vya
benki kwa kipindi cha miaka kumi ijayo ni kujenga mazingira ya kuwa na
uchumi imara na endelevu,usimamizi wa maliasili za bara la Afrika na
ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha zaidi wanawake na vijana katika ukuaji
wa uchumi wa bara la Afrika.
Katika
kuhakikisha maendeleo ya Bara la Afrika yanafikiwa kupitia Benki ya
Maendeleo ya Afrika kwa kipindi cha miaka 50 ijayo ni pamoka na
kusimamia utekelezaji wa mpango wa ‘Afrika 50’ ambao utapelekea kuongeza
ufadhili wa kiasi cha Dola bilioni 100 ambazo zinahitajika katika
kuimarisha miundombinu ya Bara la Afrika.
Awali
katika mkutano uliofanyika kati ya Mkurugenzi wa AfDB kanda ya Afrika
Mashariki Nd. Gabriel Negatu na ujumbe wa Tanzania, Katibu Mkuu Wizara
ya Fedha Dkt.Servacius Likwelile aliishukuru benki kwa jitihada zake za
kuhakikisha Tanzania inatekeleza kwa ufanisi miradi yote inayofadhiliwa
na Benki hiyo. ‘Tanzania ni miongoni mwa nchi chache Barani Afrika
ambayo inanufaika na fedha kutoka benki ya Maendeleo ya Afrika,kwa sasa
tuna zaidi ya miradi 31 ambayo inatekelezwa na AfDB’ alisema
Dkt.Likwilile.
Mwishoni
mwa Mkutano wa Magavana wa Benki,Pia walipitisha kuanzishwa kwa ‘Africa
Growing Together Fund (AGTF)’,na kiasi cha dola bilioni 2 zitatolewa na
china ili kuwezesha AfDB kukabiliana na kuongezeka kwa mahitaji ya
kikanda kwa nchi wanachama wa benki na wateja wa sekta binafsi.
Mkutano
ujao wa mwaka wa benki ya maendeleo ya Afrika utafanyika Jijini
Abidjan,nchini Ivory coast ambayo pia itakuwa mwenyeji wa maadhimisho ya
miaka 50 ya benki ya maendeleo ya Afrika yatakayoadhimishwa
Novemba,2015.
0 comments:
Post a Comment