HANDENI NA MAENDELEO YA KILIMO NA UFUGAJI
MMoja
ya wakulima wa Mahindi Wilaya ya Handeni mkoani Tanga Bw. Adalbertus
Bubelwa wa pili kutoka kushoto akimwelezea Mkuu wa wilaya ya handeni Bw.
Muhingo Rweyemamu, jinsi alivyoandaa shamba lake. Mkuu huyo wa wilaya
alikuwa katika ziara ya kuwatembelea wakulima katika vijiji mbalimbali
wilayani humo kuangalia mazao mashambani.
Mkuu
wa wilaya ya Handeni Bw. Muhingo Rweyemamu, kushoto ambaye ni mwenye
shamba akipata maelekezo kutoka kwa Afisa Kilimo wa Wilaya hiyo Bw.
Yibarik Chiza, aliyemtembelea Mkuu huyo wa wilaya shambani kwake
Afisa
Kilimo wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga Bw. Yibarik Chiza, kulia
akiwaelekeza jambo wakulima wa zao la ufuta wa Kijiji cha Misima
wilayani humo.
Mkuu
wa wilaya ya handeni Bw. Muhingo Rweyemamu, akisalimiana na mmoja wa
wananchi alipotembelea katika kijiji cha Kang’anta kuangalia maendeleo
ya mdada wa mifugo na mazao ya chakula na biashara.
Mmoja
wa wakulima wa nanasi wilayani Handeni Bi Sabrina Rory Sasumua,
akionyesha aina ya nanasi lenye uzito wa kilo mbini na nusu kutoka
katika shambani lake eneo la Kwamsisi wilayani Handeni.
Baadhi ya akina mama wa eneo la Soni katika wilaya ya Lushoto mkoani Tanga wakifanya biashara za matunda na mbogamboga.
Na Mohammed Mhina, Handeni.
WILAYA ya Handeni mkoani Tanga imetangaza kuwa haitaomba tena
chakula cha mtaada kutoka serikali kuu kwa msimu ujao kutokana na
matarajio ya kuvuna kiasi kingi cha mazao yakiwemo mahindi na ufuta
ikilinganishwa na miaka mingine iliyopita.
Mkuu wa wilaya ya Hendeni mkoani Tanga Bw. Muhingo Rweyemamu
alitoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kuwatembelea wakulima katika
vijiji mbalimbali vya wilaya hiyo kuangalia utekelezaji wa maagizo ya
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo ya kumtaka kila mwananchi
kulima kwa bidii na kupanda kwa kufuata maelekezo ya wataalam.
Akiwa katika mashamba ya wakulima wa vijiji vya Manga, Kwamsisi,
Kang’anta, Madebe, Misima, Sindeni, Mzeri na Mbagwi wilatyani Handeni,
Mkuu huyo wa wilaya Bw. Rweyemamu alisema katika msimu ijao, wilaya hiyo
haitaomba tena chakula cha msaada kwa vile wana uhakika wa kuvuna
chakula cha kutosha.
Amesema pamoja na kwamba mvua zinazoendelea kunyesha nchini kote
zimekuwa zikileta madhara kwa baadhi ya maeneo, lakini kwa wilaya ya
Handeni mvua hizo zimeleta neema na faraja kwa wakulima kutokana na
kuimarika kwa mazao yao mashambani.
Bw. Rweyemamu amesema karibu ya maeneo mengi wilayani humo, wamepata mavuno ya kutosha hasa mahindi na ufuta.
Naye Afisa Kilimo wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga Bw. Yibarik
Chiza, amesema kuwa wakulima wengi katika wilaya hiyo wamelima kwa
kutumia trekta na majembe ya kukokotwa kwa wanyamakazi jambo ambalo
amesema litawaongezea ufanisi mkubwa msimu huu.
Na kwa upande wao baadhi ya wakul;ima wilayani humo wamesema
chakula kitakachopatikana msimu huu wilayani humo hakijawahi kupatikana
zaidi ya miaka 30 iliyopita.
Shamba la mahindi katika kijiji cha Manga likionekana kustawi vya kutosha.
(Picha Zote na Mohammed Mhina)
0 comments:
Post a Comment