KLABU
ya Atletico Madrid itapambana kuhakikisha wachezaji wake bora na
inatumai kwa umuhimu wao jatika klabu na kwa kocha wao, Diego Simeone
itasaidia wakibaki.
Kipa
wa Chelsea anayecheza kwao kwa mkopo, Thibaut Courtois amezungumzia
mustakabali wake baada ya kufungwa Real Madrid 4-1 katika fainali ya
Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini kwa kiasi kikubwa hayuko mikononi mwa
Atletico.
"Sina
mawasiliano ya moja kwa moja na Chelsea,"amesema kipa huyo mwenye umri
wa miaka 22, Courtois. "Sina lolote dhidi yao. Ni kwamba nina dhamana
hii na Atletico, baada ya yote nimeishi na klabu hii kwa misimu mitatu
iliyopita,".
Hauzwi; Atletico Madrid imesema haina mpango wa kumuuza Diego Costa kulia |
Mikono salama: Kipa Thibaut Courtois amesema hana mawasiliano ya moja kwa moja na Chelsea
"Ikiwa
nitatakiwa kurudi Chelsea tu kwa ajili ya kucheza mechi za Kombe la FA
na Kombe la Ligi, nitaangalia mazingira," amesema.
Mtendaji Mkuu wa Atletico, Miguel Angel Gil Marin, amesema kwamba Diego Costa atauzwa iwapo tu atataka mwenyewe kuondoka.
Gil
amesema: "Tutajaribu kuhakikisha kwamba wachezaji wore muhimu wanabaki
hapa. Tumezungumza vizuri sana na Diego abaci na tunataka kutimiza ndoto
hii, lakini itategemea na yeye mwenyewe,".
"Lengo
letu ni kutouza mchezaji yeyote labda yule ambaye ataomba mwenyewe
kuuzwa. Kwa sababu ya mafanikio yeti katika Ligi ya Mabingwa, tuna fedha
maana yake hatuhitaji kuuza mchezaji,"amesema.
Kiungo
Koke na beki wa kushoto, Filipe Luis ni wachezaji winging wanaozitoa
udenda klabu za Ligi Kuu ya England. Lakini Koke ni kipenzi cha klabu
hiyo na Filipe Luis na rafiki wa kocha Simeone, hali ambayo inaweza
kuwafanya wabaki.
Simeone amesema: "Tutakuwa na mapumziko ya kutosha, kuangalia Kombe la Dunia na kisha tutarejea kutetea ubingwa wetu wa Ligi,".
0 comments:
Post a Comment