TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 23.05.2014.
- VYUMBA KUMI VYATEKETEA KWA MOTO KUTOKANA NA AJALI YA MOTO.
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATANO KWA KUNYWA POMBE BAADA YA MUDA.
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA WATU WATATU KWA KUKAMATWA NA SILAHA MBILI AINA YA GOBOLE.
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA KWA KUKUTWA NA BHANGI.
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA KWA KUKUTWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI[GONGO].
TUKIO LA KWANZA.
VYUMBA KUMI VYATEKETEA KWA MOTO KUTOKANA NA AJALI YA MOTO.
KIJANA MMOJA ERICK ROGERS [17]
MWANAFUNZI, MKAZI WA MANGA –VETA ALIGUNDUA KUUNGUA MOTO KWA NYUMBA YAO
NA KUTEKETEZA MALI ZOTE ZILIZOKUWA KATIKA VYUMBA KUMI [10] VYA NYUMBA
HIYO.
TUKIO HILO LILITOKEA TAREHE
22.05.2014 MAJIRA YA SAA 21:50HRS USIKU HUKO KATIKA ENEO LA MANGA –
VETA KATA YA ILOMBA,TARAFA YA IYUNGA JIJINI MBEYA. CHANZO CHA TUKIO
HILO KINACHUNGUZWA INGAWA UCHUNGUZI WA AWALI UNAONYESHA NI HITILAFU YA
UMEME KATIKA CHUMBA KILICHOKUWA NA MASHINE YA KUTOTOLESHEA VIFARANGA
VYA KUKU. HATA HIVYO MOTO HUO ULIZIMWA KWA USHIRIKIANO KATI YA KIKOSI
CHA ZIMA MOTO NA UOKOAJI,POLISI NA WANANCHI. AIDHA KATIKA TUKIO HILO
MMILIKI WA NYUMBA HIYO ROGERS SHIPELA [56] AKIWA KATIKA HARAKA ZA KUZIMA
MOTO ALIANGUKIWA NA TOFALI MGONGONI NA KUKIMBIZWA HOSPITALINI AMBAPO
ALIPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA. THAMANI HALISI YA MALI ILIYOTEKETEA
BADO KUFAHAMIKA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUWA MAKINI NA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA MAJANGA YA MOTO.
KATIKA MSAKO.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAWASHIKILIA WATU 10 KUTOKANA NA MISAKO MBALIMBALI ILIYOFANYIKA.
KATIKA TUKIO LA KWANZA JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WATU WATANO
KWA KUKUTWA WAKINYWA POMBE BAADA YA MUDA KWISHA, WATUHUMIWA HAO NI 1.
MATASHA ZUBERI [38],MKAZI WA MTAA WA BENK 2. VICK MICHAEL [29]MKAZI WA
MTAA WA BENK, 3. YUSUPH MWANSASU [30], MKAZI WA JUAKALI 4. NGOME
SANGA [33], MKAZI WA MWANJELWA NA 5. OLI MAULID [30],MKAZI WA
MWANJELWA.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE
22.05.2014 MAJIRA YA SAA 23:45HRS USIKU KATIKA KILABU CHA POMBE
KIITWACHO KINGANI-UYOLE KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA. TARATIBU
ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI.
KATIKA TUKIO LA PILI JESHI LA
POLISI LIMEMKAMATA PETER DAIMON [25] MKAZI WA MLIMA RELI-MBALIZI AKIWA
NA BHANGI YENYE UZITO WA GRAM 256.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE
22.05.2014 MAJIRA YA SAA 13:30HRS MCHANA HUKO KATIKA ENEO LA
MSHIKAMANO, KATA YA UTENGULE-USONGWE, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI.
TARATIBU ZINAFANYWA ILIAFIKISHWE MAHAKAMANI.
KATIKA TUKIO LA TATU JESHI LA
POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA MAAFISA WA WANYAMAPORI WA PORI LA
MITUNDU-RUNGWA WALIWAKAMATA WATU WATATU WAKIWA NA SILAHA BUNDUKI MBILI
AINA YA GOBOLE BILA KIBALI. WATUHUMIWA HAO NI 1. EMANUEL CHAPA [42] 2 .
MASHAKA PATRICK [39] NA 3. ABRAHAM MWAITURO [58] WOTE WAKAZI WA
KIJIJI CHA NKUNG’UNGU-LUPA WILAYA YA CHUNYA.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE
21.05.2014 MAJIRA YA SAA 05:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA
NKUNG’UNGU,KATA YA LUPA,TARAFA YA KIPEMBAWE WILAYA YA CHUNYA MKOA WA
MBEYA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI.
AIDHA KATIKA TUKIO LA NNE JESHI
LA POLISI LIMEFANIKIWA KUMKAMATA TUMPE EDWARD [28], MKAZI WA MAPELELE
AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 1.5
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE
22.05.2014 MAJIRA YA SAA 17:30HRS JIONI NA HUKO KATIKA MAENEO YA
DDC-MBALIZI, KATA YA MBALIZI, TARAFA YA BONDE LA USONGWE WILAYA YA
MBEYA VIJIJINI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA NA POMBE
HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA
MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA
MAMLAKA HUSIKA JUU YA MTU/WATU WANAOMILIKI SILAHA BILA KIBALI IKIWA NI
PAMOJA NA WAWINDAJI HARAMU ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE
MARA MOJA.
Signed by:
[ AHMED Z. MSANGI – SACP ].
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment