Na Baraka Mpenja,
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa
Tanzania anayeichezea klabu ya TP Mazembe ya DR Congo, Mbwana Ally
Samatta yuko hatihati kuichezea timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars
katika mchezo wa marudiano kesho kutwa (jumapili) dhidi ya Zimbabwe,
mjini Harare, kuwania kupangwa hatua ya makundi kusaka tiketi ya
kushiriki kombe la mataifa ya Afrika, AFCON mwakani nchini Morocco.
Taarifa za uhakika ni kwamba
Samatta alipata majeruhi ya nyama za paja katika mechi ya ligi ya
mabingwa barani Afrika mei 25 mwaka huu dhidi ya wapinzani wao AS Vita
mjini Lubumbashi, huku akifunga bao pekee katika ushindi wa TP Mazembe
wa bao 1-0. Katika mchezo huo, Samatta alitolewa dakika ya 75 kutokana
na majeruhi hayo.
Hata hivyo imeelezwa kuwa
shirikisho la soka Tanzania, TFF, baada ya kuambiwa na TP Mazembe kuwa
Samatta ni majeruhi, wao walilazimisha kumtumia mchezaji huyo.
Ili kusoma mahojiano yote yaliyofanyika baina ya mwandishi na meneja wa Samatta bofya www.bkmtata.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment