Friday, 23 May 2014

TAARIFA YA POLISI KUHUSU VIKUNDI VYA MBWA MWITU

adverasenso
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI 
Kufutia kuibuka kwa vikundi vya vijana vinavyojulikana kwa majina ya mbwa mwitu, watoto wa mbwa au Panya road na kujihusisha na vitendo vya kihalifu ikiwemo uporaji, unyang’anyi wa kutumia nguvu na kujeruhi watu katika maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam, Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi (DIGP) Abdulrahaman Kaniki amewaagiza makamanda hususani wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam kuhakikisha wanavitafuta vikundi hivyo popote vilipo, kuwakamata na kuwafisha katika vyombo vya sheria.
Naibu IGP amekemea vikali vikundi hivyo na kuvitaka kuacha tabia hiyo mara moja, kwani vitendo hivyo ni vya kihalifu na vinatakiwa kukemewa na kila mtu katika jamii.
Aidha, amewataka wananchi kuondoa hofu na badala yake watoe ushirikiano kwa kutoa taarifa za vikundi hivyo katika vituo vya Polisi ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa.
Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

0 comments: