Dkt. Damas Daniel Ndumbaro |
Imechapishwa Mei 25, 2014, saa 8: 20 usiku
KAMATI ya uchaguzi ya klabu ya Simba sc leo
inatarajia kuanza kusikiliza mapingamizi ya wagombea wa nafasi mbalimbali za
uongozi kuanzia majira ya saa 3:00 asubuhi katika ukumbi wa Gymkan jijini Dar
es salaam.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mwanasheria na wakala
wa wachezaji wa FIFA, Dkt. Damas Daniel Ndumbaro amesema zoezi hilo
litazingatia haki kwasababu kamati yake inajumuisha watu makini na wenye
malengo ya kuipatia Simba sc viongozi bora.
“Msimamo wetu uko pale pale, sisi hatumuondoa
mgombea, bali kanuni za uchaguzi za TFF na katiba ya Simba ndio itamuondoa
mgombea”. Alisema Ndumbaro.
Ndumbaro aliongeza kuwa wanasimba wawe na imani na
kamati yake kwasababu haitapindisha sheria na kanuni hata kidogo.
Aidha, Ndumbaro alisema watu wote waliowawekea
pingamizi wagombea wanatakiwa kufika muda uliotajwa wakiwa na viambatanisho
vyote hususani vithibitisho vya pingamizi zao.
“Tulishawaandikia barua watu wote walioweka
mapingamizi na kuwaeleza kila kitu. Lazima wawepo wakati wa kusikilizwa kwa
mapingamizi yao kama sheria inavyotaka”.
“Kama mtu hatakuwepo, pingamizi lake
halitasikilizwa” . Alisema Ndumbaro.
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
0 comments:
Post a Comment