TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 31.05.2014.
- MWANAMKE MMOJA AUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI NA MUME WAKE.
- MTU MMOJA AUAWA NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWA TUHUMA ZA WIZI.
- MWANAFUNZI WA DARASA LA TATU AFARIKI DUNIA BAADA YA KUDONDOKA NA KISHA KUKANYAGWA NA POWERTILLER.
- MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WANNE KUTOKANA NA TUHUMA MBALIMBALI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MWANAMKE MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA
JINA LA CHRISTINA HAYOLA (35) MKAZI WA KIJIJI CHA LIWALANJE, ALIKUTWA
AMEUAWA KWA KUKATWA KITU CHENYE NCHA KALI KICHWANI, KIFUANI NA MGUU WA
KULIA NA MUME WAKE AITWAYE MUSSA NSAGAJE @ MWAULAMBO.
MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA MNAMO
TAREHE 30.05.2014 MAJIRA YA SAA 06:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA
MAGAMBA, KATA YA ISANZA, TARAFA YA IGAMBA, WILAYA YA MBOZI MKOA WA
MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI UGOMVI ULIOTOKANA NA WIVU
WA KIMAPENZI ULIOTOKEA WAKIWA KILABUNI USIKU.
MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO. JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE
KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE
DHIDI YAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA
KWA JINA LA ABDI SANGA (20) MKAZI WA ISANGA ALIUAWA KWA KUPIGWA SEHEMU
MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA
SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI FIMBO, MAWE NA RUNGU.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE
31.05.2014 MAJIRA YA SAA 03:45 USIKU WA KUAMKIA LEO HUKO ENEO LA FOREST
YA ZAMANI KATA YA FOREST, TARAFA YA SISIMBA JIJI NA MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILI NI TUHUMA ZA WIZI BAADA YA MAREHEMU
NA MWENZAKE MMOJA AMBAYE ALIFANIKIWA KUKIMBIA KUINGIA NYUMBANI KWA
KASSIM ISSA (28) MKAZI WA FOREST NA KUIBA VITENGE VYENYE THAMANI YA
TSHS 70,000/=, MHANGA ALIPIGA KELELE ZA KUOMBA MSAADA, HIVYO KUNDI LA
WATU WALIJITOKEZA NA KUMSHAMBULIA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA
SHERIA NA INA MADHARA MAKUBWA NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA
WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA
ZAIDI ZA KISHERIA.
KATIKA TUKIO LA TATU:
MWANAFUNZI
WA DARASA LA TATU KATIKA SHULE YA MSINGI IBUMILA ALIYETAMBULIKA KWA
JINA LA FATINA FESTO @ MWANDOSYA (12) MKAZI WA KIJIJI CHA MAHONGOLE
ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUDONDOKA KUTOKA KWENYE POWER
TILLER ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA AIZACK MWASHANGWA (22) MKAZI WA
MAHONGOLE.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE
30.05.2014 MAJIRA YA SAA 15:30 ALASIRI HUKO KATIKA KIJIJI CHA
IBUMILA-MAHONGOLE, KATA YA SONGWE-IMALILO, TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA
MBARALI, MKOA WA MBEYA. WAKATI TUKIO HILO LINATOKEA MAREHEMU NA WENZAKE
WALIKUWA WANATOKA KUVUNA MPUNGA WA SHULE. CHANZO CHA AJALI
KINACHUNGUZWA. DEREVA ALIKIMBIA NA KUACHA POWER TILLER MARA BAADA YA
TUKIO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA [DEREVA] AZITOE KATIKA
MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE,
VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.
KATIKA TUKIO LA NNE:
MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI
KATIKA SHULE YA SEKONDARI MAKONGOLOSI ALIYEMBALIWA KWA JINA LA ADEN
PETER @NGOMBE (17) MKAZI WA MAKONGOLOSI AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA
YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.117 APK/T.150 AVM AINA YA
SCANIA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE ALLY MOSHI (35) MKAZI
WA MBARALI.
TUKIO HILO LA AJALI LIMETOKEA
MNAMO TAREHE 30.05.2014 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI NA
KATA YA MAKONGOLOSI, TARAFA YA KIWANJA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA
KATIKA BARABARA YA MAKONGOLOSI/LUPA. CHANZO CHA AJALI DEREVA ALIKUWA
AMELEWAPOMBE. MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUO CHA POLISI –
MAKONGOLOSI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WATUMIAPO VYOMBO VYA MOTO HASA KWA KUZINGATIA
SHERIA NA ALAMA ZA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI. AIDHA ANAENDELEA KUTOA
WITO KWA WATEMBEA KWA MIGUU KUFUATA NA KUZINGATIA ALAMA ZA USALAMA
BARABARANI IKIWA NI PAMOJA NA KUTEMBEA PEMBENI MWA BARABARA NA KUVUKA
KATIKA MAENEO YENYE VIVUKO VYA KUVUKIA ILI KUEPUKA AJALI
TAARIFA YA MISAKO:
KATIKA MSAKO WA KWANZA:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MWIYULEGHE MBUGHI (60)
MKAZI WA KIJIJI CHA ITENTULA AKIWA ANAMILIKI BILA KIBALI SILAHA
/BASTOLA MOJA AINA YA BABY YENYE NAMBA 946663 ILIYOTENGENEZWA NCHINI
UBELGIJI IKIWA NA RISASI TATU [03] KWENYE MAGAZINE.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE
30.05.2014 MAJIRA YA SAA 01:00 USIKU WA KUAMKIA LEO HUKO KATIKA KIJIJI
CHA ITENTULA, KATA YA BARA, TARAFA YA ITAKA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA
MBEYA. MTUHUMIWA ALIKUWA AMEKUFICHA SILAHA HIYO CHUMBANI NDANI YA
NYUMBA YAKE. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
KWA JAMII KUACHA KUJIMILIKISHA SILAHA KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE
WAFUATE TARATIBU ZA UMILIKAJI WA SILAHA KIHALALI.
KATIKA MSAKO WA PILI:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA DEZDERIS JACKSON (30)
MKAZI WA KIJIJI CHA SAZA AKIWA NA KETE 17 ZA BHANGI KWENYE KIBANDA CHA
KUUZA SABUNI SAWA NA UZITO WA GRAM 85.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE
30.05.2014 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA SAZA, KATA
YA MKWAJUNI, TARAFA YA KWIMBA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
MTUHUMIWA NI MTUMIAJI NA MUUZAJI WA BHANGI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI
HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
KATIKA MSAKO WA TATU:
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA
LA EVA WILSON (23) MKAZI WA KIJIJI CHA BWAWANI ANASHIKILIWA NA JESHI LA
POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA ANAUZA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA
SERIKALI[VIROBA] AINA YA BOSS PAKETI 51.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE
30.05.2014 MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA HUKO KATIKA KITONGOJI NA KIJIJI
CHA BWAWANI, KATA YA MAKONGOLOSI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA,
MKOA WA MBEYA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII HASA WAFANYABIASHARA KUACHA KUJIHUSISHA NA UUZAJI WA BIDHAA
ZILIZOPIGWA MARUKUFU NA SERIKALI KWANI ZINA MADHARA KIAFYA KWA
WATUMIAJI.
KATIKA MSAKO WA NNE:
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA
LA ESTER MWALUGAJA (34) MKAZI WA KIJIJI CHA MAMBA-F ANASHIKILIWA NA
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO]
UJAZO WA LITA MBILI [02].
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE
30.05.2014 MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MTANDE,
KIJIJI CHA MAMBA -F, KATA YA MAMBA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA
CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA
WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA
WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO
KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA ZA WATU WANAOJIHUSISHA NA MTENGENEZAJI
NA UUZAJI WA POMBE HARAMU YA MOSHI.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment