Wananchi
wakifuatilia mkutano wa hadhara wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa)
uliofanyika juzi eneo la Polisi Nguruka, Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.
Picha na Ibrahim Yamola
Wakati
Polisi mkoani Kigoma wakiwa wamemtia nguvuni Katibu Mkuu wa chama cha
NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe kwa tuhuma ya kumdhalilisha Rais Jakaya
Kikwete, Kiongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Profesa
Ibrahimu Lipumba amesema hawatarudi bungeni mpaka kiongozi huyo wa nchi
aombe radhi.
Nyambabe
alikamatwa juzi saa 5 usiku katika Kijiji cha Nguruka Wilaya ya Uvinza
mkoani humo saa kadhaa baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara wa
UKAWA uliohutubiwa na Nyambabe na viongozi kutoka vyama vya Chadema na
CUF.
Akiwahutubia
mamia ya wakazi wa Nguruka katika mkutano wa Ukawa wenye lengo la
kuwaelimisha wananchi kuhusu mchakato wa Katiba, Nyambabe alisema Rasimu
ya Katiba ikipita kuwa Katiba, mamlaka ya uteuzi wa ovyo haitakuwapo
tena.
"Jaji
Warioba (aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba) ameweka
mamlaka ya uteuzi kwenye Rasimu ya Katiba na Rais hataweza tena kuteua
marafiki zake, shemeji zake, watu wake wa karibu kuwa viongozi
mbalimbali hadi taratibu za ajira zifuatwe.
"Hivi
sasa kuna mawaziri mizigo walioteuliwa na Rais (Kikwete) ambao
wanalalamikiwa na chama chake (CCM) kushindwa kutekeleza majukumu yao na
hii inatokana na kupeana madaraka kwa njia zisizo stahili," alisema
Nyambabe.
Polisi wamdaka
Baada ya
kumalizika mkutano huo, Nyambabe akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa
Vijana Taifa wa Chadema, John Heche na Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF,
Ashura Mustapha walikwenda hoteli waliyofikia ya New Gevena.
Ilipofika
saa 5 usiku askari kanzu wanne walifika hotelini hapo wakiwataka
viongozi hao kwenda Kituo cha Polisi Nguruka kwa madai ya kufanya
uchochezi.
Walipofika
walimwambia mhudumu wa hoteli hiyo kuwa wanawataka viongozi hao na
aliwajibu hawapo jambo lililowafanya kumtaka kuwapa kitabu cha wageni wa
siku hiyo.
Walipopewa kitabu walikuta jina la Nyambabe kuwapo hotelini hapo, Heche na Ashura wakiwa wameondoka kwenda Kigoma Mjini.
"Wakati
askari hao wanne wapo ndani ya hoteli, nje kulikuwa na askari sita wenye
silaha wakiwa wameizunguka hoteli hiyo na kumchukua kisha kwenda naye
moja kwa moja Kituo cha Polisi Nguruka," alisema Mohamed Mtulya ambaye
ni Ofisa Usalama wa NCCR-Mageuzi.
CHANZO:MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment