Mbu hawa wananofiwa kuanza kusababisha Malaria
Viini vinavyosababisha Malaria
Utafiti uliofanywa nchini Uingereza unaonyesha kuwa Mbu wameanza kuvamia maeneo mbali mbali ya nchi hiyo.
Mabadiliko katika hewa ya mjini nchini
Uingereza yameanza kutoa mazingira mazuri kwa Mbbu kuishi, ikiwemo wale
wenye uwezo wa kuambukiza ugonjwa wa Malaria na virusi vijulikanavyo
kama 'West Nile virus'.Utafiti unasema kuwa mazingira ya joto pamoja na vidimbwi vya maji katika nyumba za watu, yanawaleta Mbu karibu na watu.
Mbu wanaopatikana nchini Uingereza hawana uwezo wa kuambukiza maradhi yoyote, lakini wanasayansi hao wanasema kuwa jambo la wadudu hao kuzaana katika maeneo ya mjini linaongeza uwezo wa magonjwa kulipuka.
Wanasayansi hao hata hivyo wanakusanya data zaidi kuona ikiwa wengi wa wadudu pamoja na aina ya wadudu wenyewe inaweza kuchangia kwa vyovyote mlipuko wa maradhi au la, hasa katika maeneo ya mjini.
Kadhalika wanasayansi hao wanasema kuwa kutokana na ongezeko la viwango vya joto katika maeneo ya mjini,Mbu katika baadhi ya maeneo kama vile Kusini mwa Ulaya wameweza kusababisha magonjwa.
Pia wanasisitiza kwamba Magonjwa yamelipuka katika baadhi ya mataifa ya Ulaya kutokana na mabadiliko ya tabia ya Mbu.
Zaidi ya aina 30 ya Mmbu wamepatikana nchini Uingereza
"katika maeneo ya vijijini kuna Mmbu wengi zaidi kwa sababu ya mazingira tofauti tofauti, wengine wanapenda kuishi katika nyasi , wengine katika vidimbwi, na wengine katika mashimo,'' alisema mmoja wa wataalamu.
"lakini ukienda katika maeneo ya mijini , hakuna Mmbu wengi sana , labda utapa aina mbili au tatu ya Mmbu.
Daktari mmoja kwa jina Callaghan, alisema kuwa kulikuwa na visa vingi vya ugonjwa wa Malaria kila mwaka nchini Uingereza , wengi wanaokuwa wanarejea kutoka sehemu mbali mbali za dunia ambako ugonjwa Malaria unapatikana.CHANZO BBC
0 comments:
Post a Comment